HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

September 15, 2017

Mikakati ya TGNP baada ya Tamasha la Jinsia 2017

Mshauri mwandamizi kutoka Shirika la UN Women, Bi. Usu Mallya (kulia) akiwasilisha mada kwenye Tamasha la Jinsia Tanzania 2017. Mwanaharakati mkongwe Gema Akilimali (kushoto) akiwasilisha mada kwenye Tamasha la Jinsia Tanzania 2017. Wengine ni maofisa maendeleo ya jamii wakifuatilia. Mwenyekiti wa Bodi ya TGNP, Vicensia Shule akizungumza kwenye Tamasha la Jinsia Tanzania Mwaka 2017. Mwanaharakati na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Wanawake Tanzania (WFT), Mary Rusimbi akizungumza kwenye moja ya warsha katika Tamasha la Jinsia Tanzania 2017.[/caption] KUANZIA Septemba 5 hadi 8, 2017 Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa masuala ya jinsia iliadhimisha siku nne za Tamasha la 14 la Jinsia Tanzania. Siku hizo nne ziliambatana na shughuli za sherehe, tafakuri, mijadala na pongezi. Baada ya kumalizika kwa shughuli zote hizo TGNP Mtandao na wadau washiriki katika tamasha walitoka na mikakati kadhaa kukabiliana na changamoto zilizoibuliwa. Bi. Vicensia Shule ni Mwenyekiti wa Bodi ya TGNP Mtandao, anasema baada ya tamasha hilo mikakati waliojiwekea kukabiliana na changamoto zilizoibuliwa ni pamoja na kushirikisha wadau mbalimbali zikiwemo AZAKI, wadau wa maendeleo, asasi za elimu ya juu na taasisi za Serikali katika kutafuta na kufanya uchambuzi ili ili kupata taarifa na takwimu sahihi juu ya mimba na ndoa za utotoni, ukatili wa kijinsia na umiliki wa ardhi kwa wanawake na watu wenye ulemavu. Anasema pia wataendelea kuimarisha mikakati ya kuweka kumbukumbu za wanawake waliotoa michango katika maendeleo kwenye nyanja mbalimbali na kusambaza taarifa za kumbukumbu hizo kwa ajili ya watu kujifunza na kuwaenzi wanawake hao. Pia kupanua wigo wa kutoa mafunzo ya kimwongozo katika kuchukua na kuhifadhi kumbukumbu za wanawake kwa AZAKI, vijana na wadau wengine. Aidha Bi. Vicensia Shule anaeleza kuwa mikakati mingine ni kuweka mipango endelevu wa kurithisha ujuzi na maarifa kutoka kizazi/rika moja kwenda nyingine, hasa kutoka kwa wanawake waliobobea kwenye tasnia mbalimbali. Pamoja na hayo anasema mkakati mwingine ni kushinikiza sera na mipango ya Serikali iingize masuala ya vijana ili waweze kushiriki kikamilifu katika maendeleo nyanja zote, hii ni kwa kuwa zaidi ya asilimia 60 ya Watanzania ni vijana. Watashawishi pia rasilimali za kutosha zitengwe ili kuwezesha utekelezwaji wa mipango na mikakati ya vijana bila kujali itikadi, jinsi, dini, jiografia na hali ya kipato.  
Baadhi ya washiriki kwenye Tamasha la Jinsia Tanzania Mwaka 2017. Baadhi ya washiriki kwenye Tamasha la Jinsia Tanzania Mwaka 2017. Baadhi ya washiriki kwenye Tamasha la Jinsia Tanzania Mwaka 2017. Afisa Maendeleo ya Jamii, Halmashauri ya Mbeya, Zena Kapama akizungumza katika moja ya warsha kwenye Tamasha la 14 la Jinsia Tanzania. 
Mratibu wa MVIWATA Kyela, Bi. Theodora Pius akichangia hoja katika Tamasha la 14 la Jinsia Tanzania. Mjumbe Kamati ya Ushauri katika Mfuko wa Wanawake Tanzania (WFT), Dk. Dinah Mmbega akichangia hoja kwenye moja ya warsha katika Tamasha la Jinsia Tanzania 2017.

No comments:

Post a Comment

Pages