Tundu Lissu |
Akizungumza na waandishi wa habari mjini Dodoma, Kiongozi wa Kambi Rasmi Bungeni na Mbunge wa Hai, Freeman Mbowe, amesema kuwa 'Lissu ameshambuliwa na watu waliokuwa wakilufuata gari lake kwa nyuma na kutoa bunduki aina ya SMG na kupiga risasi nyingi gari lake na kusababisha majeraha makubwa mwilini mwake. Tukio hilo limetokea majira ya saa saba mchana
Naye Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba, amesema kuwa 'tumuombe Mungu mambo haya yasiendelee'
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma amewataka wananchi wasikusanyike nje ya Hospitali ya Mkoa wakati Mbunge huyo akipata matibabu ya dharura katika Hospitali ya Mkoa wa Dodoma.
Habari zaidi zinasema kuwa Mh. Tundu Lissu anatarajiwa kusafirishwa kwa ndege kuja jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kupata matibabu zaidi katika hospitali ya Taifa Muhimbili.
Wakati huohuo Rais John Magufuli ameandika katika mtandao wake wa Twitter 'Nimepokea kwa masikitiko tukio la kupigwa risasi Mh. Tundu Lissu, namuombea kwa Mwenyezi Mungu aweze kupona haraka. 1/2
Aidha, vyombo vya dola viwasake wale wote waliohusika na tukio hili la kinyama na kuwafikisha katika mikono ya sheria.2/2

No comments:
Post a Comment