Mkurugenzi wa Kampuni ya Udalali ya Msama, Alex Msama, akizungumza na
waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Novemba 27, 2017 kuhusu zoezi ya kuwakamata
watu wanaojihusisha na uuzaji wa CD feki za wasanii ambapo zoezi hilo
litahamia katika Mkoa wa Morogoro baada ya kufanyika kwa mafanikio
makubwa jijini Dar es Salaam. (Picha na Francis Dande).
Mkurugenzi wa Kampuni ya Udalali ya Msama, Alex Msama, akizungumza na
waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Novemba 27, 2017. (Picha na Francis Dande).
NA MWANDISHI WETU
KAMPUNI ya Udalali ya Msama Auction Mart ya jijini Dar es Salaam, imepata mafanikio makubwa katika mkakati wake wa kukabili biashara ya kazi feki za wasanii katika maeneo mbalimbali ya jiji hilo.
Hayo yalisemwa jana na Mkurugenzi wa kampuni hiyo, Alex Msama wakati akielezea mafanikio na changamoto kadhaa zilizojitokeza katika zoezi linaloendelea kwa jiji hilo.
Alisema tangu kuanza kwa kamatakamata ya kazi feki na kazi zilizoingia sokoni bila stika za Mamlaka ya Mapato Tanzania, wamepata mafanikio makubwa japo ni kero kwa wahusika.
Kuhusu mafanikio, Msama aliyechangia kwa kiasi kikubwa mafanikio ya muziki wa injili kwa nchini za ukanda wa Afrika Mashariki, alisema wamewakamata wengi wenye kufanya biashara hiyo haramu.
“Tumekamata zaidi ya watu 200 ambao wataburuzwa mahakamani hivi karibuni baada ya taratibu kukamilika na vifaa vingi kama kompyuta, mashine za kudurufia na kazi ambazo zilikuwa sokoni,” alisema Msama.
Alisema, baada ya kamatakamata hiyo kugusa maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam na kuacha maumivu makubwa, msako huo wa aina yake utakuwa endelevu.
Kuhusu changamoto, Msama alisema ni baadhi ya wenye kunufaika na biadhara hiyo haramu, kupanga mbinu za kuipaka matope kwa madai kuwa inawabana machinga.
Msama alisema, Serikali haina tatizo na Machinga, tena inawapenda mno, lakini ni yule anayefanya kazi yake kwa mujibu wa taratibu za nchi ikiwemo kulipa kodi kwa maslahi ya wasanii na serikali.
Msama alisema, baada ya msako huo kupiga kambi kwa muda mrefu katika mkoa wa Dar es Salaam, kuanzia wiki ijayo wataanza kuelekea mikoani wakianzia Morogoro.
Alisema mbali ya msako huo kuelekea mikoani, bado kikosi kazi kitaendelea kufanya misako ya kushtukiza hasa nyakati za usiku baada ya wahusika sasa kufanya kazi hiyo haramu nyakati hizo kukwepa kukamatwa.
Katika hatua nyingine, Msama ametoa shukrani kwa Rais John Magufuli kwa kutaka mtu ale kwa jasho lake, Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam na Jeshi la Polisi na Kamishna wa Kodi za Ndani wa TRA.

No comments:
Post a Comment