Kocha
Mkuu wa timu ya mpira wa miguu ya Tanzania Bara, ‘Kilimanjaro Stars’,
Ammy Conrad Ninje, ameongeza nyota watatu katika kikosi chake mara baada
ya Baraza la Soka la Afrika Mashariki (CECAFA), kuridhia kuongezwa
wachezaji watatu kwa kila timu.
Awali,
CECAFA ilihitaji wachezaji 20 tu, lakini sasa wameongeza watatu na
kufanya idadi mpya ya wachezaji watakaoshiriki michuano hiyo ya Chalenji
kwa mwaka huu kuwa 23.
Wachezaji
walioongezwa na Kipa Ramadhani Kabwili kutoka Young Africans ya Dar es
Salaam, Amani Kiata wa Nakuru All Stars ya Kenya na Yahya Zayd kutoka
Azam FC ya Dar es Salaam.
Kikosi
cha wachezaji 20 wa awali wa Ninje - Kocha wa Daraja ‘A’ la Shirikisho
la Mpira wa Miguu Ulaya (UEFA), ni makipa Aishi Manula (Simba SC) na
Peter Manyika (Singida United).
Walinzi
ni Gadiel Michael (Young Africans), Boniphace Maganga (Mbao FC), Kelvin
Yondani (Young Africans), Kennedy Juma (Singida United), Erasto Nyoni
(Simba SC) na Mohammed Hussein (Simba SC).
Viungo
wa kati ni Himid Mao ambaye ni Nahodha (Azam FC), Jonas Mkude (Simba
SC), Hamis Abdallah (Sony Sugar/Kenya), Mzamiru Yassin (Simba SC),
Raphael Daud (Young Africans), Shizza Kichuya (Simba SC), Abdul Hilal
(Tusker/Kenya) na Ibrahim Ajib (Young Africans).
Washambuliaji
ni Mbaraka Yussuph (Azam FC), Elias Maguri (Dhofar/Mascat, Oman),
Daniel Lyanga (Fanja FC/Mascat) na Yohana Mkomola (Ngorongoro Heroes).
Benchi
la Ufundi linaundwa na yeye Ninje ambaye ni Kocha Mkuu, Fulgence
Novatus (Kocha Msaidizi), Patrick Mwangata (Kocha wa Makipa), Danny
Msangi (Meneja), Dkt. Richard Yomba (Daktari wa timu), Dkt. Gilbert
Kigadye (Daktari wa Viungo) na Ally Ruvu (Mtunza Vifaa).
Katika
michuano hiyo inayotarajiwa kuanza Desemba 3, mwaka huu, Kilimanjaro
Stars imepangwa Kundi ‘A’ pamoja wenyeji Kenya, Rwanda na Libya ambayo
ni timu mwalikwa kutoka Kaskazini mwa Afrika.
Kilimanjaro
Stars ambayo imewahi kutwaa mara tatu taji hilo la Chalenji tangu
kuanzishwa kwake, itaaza kampeni za kurudisha heshima yake dhidi ya
Libya katika kundi hilo la A utaofanyika Desemba 3, mwaka huu.
Mashindano
ya mwaka huu CECAFA ilifikia makubaliano na kanda mbili za Kusini mwa
Afrika - COSAFA na ile ya Kaskazini UNAF kualika timu mbili za kutoka
kanda hizo na mataifa ya Libya na Zimbabwe.
Jumla
ya timu shiriki kwenye CECAFA Senior Challenge Cup mwaka huu itakuwa 10
ambazo ni pamoja na wenyeji Kenya, Uganda, Tanzania, Rwanda, Burundi,
South Sudan, Ethiopia, Zanzibar, Somalia, Zimbabwe na Libya.
Sudan wenyewe wamejiondoa katika mashindano ya mwaka huu wakati mataifa mawili ya Eritrea na Djibouti nayo hayatashiriki.
Michuano
hiyo itatumia viwanja vya Moi kilichopo Kisumu (Moi Stadium), Bukungu
kilichopo Kakamega na Afraha kilichopo Nakuru wakati Uwanja wa Kasarani
Nairobi na ule wa Kenyatta uliopo Machakos vitatumika kama viwanja vya
ziada.
Makundi 2017 Cecafa Challenge Cup
Kundi A: Kenya, Libya, Rwanda, Tanzania, Zanzibar.
Kundi B: Uganda, Zimbabwe, Burundi, Ethiopia, South Sudan.
Ratiba ya michuano hiyo mwaka huu ni kama ifuatavyo:
Desemba 3, 2017
Kundi A
Libya vs Tanzania
Kenya vs Rwanda
Desemba 4, 2017
Kundi B
Burundi vs Ethiopia
Uganda vs Zimbabwe
Desemba 5, 2017
Kundi A
Zanzibar vs Rwanda
Kenya vs Libya
Desemba 6, 2017
Kundi B
Sudan Kusini vs Zimbabwe
Uganda vs Burundi
Desemba 7, 2017
Tanzania vs Zanzibar
Rwanda vs Libya
Desemba 8, 2017
Kundi B
Sudan Kusini vs Ethiopia
Zimbabwe vs Burundi
Desemba 9, 2017
Kundi A
Rwanda vs Tanzania
Kenya vs Zanzibar
Desemba 10, 2017
Kundi B
Sudan Kusini vs Burundi
Ethiopia vs Uganda
Desemba 11, 2017
Kundi A
Libya vs Zanzibar
Kenya vs Tanzania
Desemba 12, 2017
Kundi B
Uganda vs Sudan Kusini
Zimbabwe vs Ethiopia
Desemba 13, 2017
Mapumziko
Desemba 14, 2017
Nusu fainali 1 (Mshindi Kundi A vs Mshindi wa pili Kundi B)
Desemba 15, 2017
Nusu fainali 2 (Mshindi Kundi B vs Mshindi wa pili kundi A)
Desemba 16, 2017
Mapumziko
Desemba 17, 2017
Mshindi wa Tatu & Fainali
……………………………………………………………………..…… ………..……
IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA
No comments:
Post a Comment