Mkuu wa
Majeshi ya Ulinzi Jenerali Venance Mabeyo akimkabidhi Bendera ya Taifa Nahodha wa Timu ya Wanawake ya Klabu
ya Gofu ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi
wa Tanzania ya Lugalo inayotarajia kushiriki mashindano ya Wazi ya Wanawake ya
IBB nchini Nigeria Hivi karibuni ( Picha
na Luteni Selemani Semunyu).
Mkuu wa
Majeshi ya Ulinzi Jenerali Venance Mabeyo akisalimiana na Wachezaji wa Timu ya Wanawake
ya Klabu ya Gofu ya jeshi la ulinzi la Wananchi
wa Tanzania ya Lugalo inayotarajia kushiriki mashindano ya Wazi ya Wanawake ya
IBB nchini Nigeria hivi karibuni. (Picha
na Luteni Selemani Semunyu).
Mwenyekiti wa wa
Chama cha Gofu nchini Joseph tango (aliyesimama) akizungumza wakati wa Mkutano
na Waandishi wa habari Makao Makuu ya Jeshi Upanga ambapo timu ya Wanawake ya Klabu ya Jeshi ya Lugalo
walikabidhidhwa bendera kwa ajili ya kushiriki Michuano ya Wazi nchini Nigeria
aliyeka Kushoto ni Mwenyekii wa Lugalo
Brigedia Jenerali Michael Luwongo Mstaafu. ( Picha na Luteni Selemani Semunyu).
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Venance Mabeyo akisalimiana na Afisa habari wa Klabu ya Gofu ya Jeshi ya Lugalo Luteni selemani Semunyu (kulia), baada ya
kukabidhi Bendera kwa Nahodha wa Timu ya
Wanawake ya Klabu ya Gofu ya jeshi la ulinzi la Wananchi wa tanzania ya Lugalo inayotarajia
kushiriki mashindano ya Wazi ya Wanawake ya IBB
nchini Nigeria Hivi karibuni ( Picha na Luteni Selemani Semunyu).
Na Luteni Selemani Semunyu JWTZ
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Venance Mabeyo amewataka
wachezaji wa Timu ya Wanawake ya Gofu ya Klabu ya Jeshi ya Lugalo kuhakikisha wanarejesha heshma ya
jeshi kuwa kinara katika michezo na kuzalisha wachezaji bora wanaowakilisha
nchi kwa mafaniko.
Aliyasema hayo Makao Makuu ya jeshi Upanga Jijini Dar es Salaam wakati akiagana na wachezaji Sita wa Gofu
wanaotarajia kuwakilisha nchi katika michuano ya wazi ya wanawake nchini Nigeria IBB Ladies Open Championship 2018 yanayaotarajia kufanyika hivi karibuni.
Jenerali Mabeyo alisema kama ilivyokuwa katika
Michezo ya Riadha na Ngumi sasa tunataka na kwenye gofu na kwa kuanza ni timu
hii ya Gofu ya Wanawake kuhakikisha inarudi na ushindi mnono.
“ Nikiwa mlezi wa Klabu naamini mtatuwakilisha vyema
na Jeshi kwa ujumla tutaendelea kuwaunga mkono wachezaji wa Gofu na hata Michezo mingine kuhakikisha
jeshi linaendelea kuwa kinara w michezo nchini na kuwa chachu kwa wengine”
Alisema Jenerali Mabeyo.
Aliongeza kuwa licha ya matumaini yake katika Gofu
lakini pia katika Soka licha ya Mchezo huo kutawaliwa na simba na yanga lakini
sasa walau mwanga unaonekana baada ya ya Timu ya Jeshi ya Green Worriorrs
kuifurusha Timu ya Simba katika Michuano ya Kombe la Shirirkisho.
“Ushindi ule ulikuwa Mwanzo mzuri wa kupunguza Ubabe
wa Simba na Yanga na Ushabiki wa Simba na Yanga hata miongoni mwa Wachezaji
hivyo nanyi kama mlivyofanya vyema katika mashindano Uganda sasa tunatarajia
Ushindi toka Nigeria” Alisema Jenerali Mabeyo.
Kwa Upande wa mwenyekiti wa Klabu hiyo Brigedia
Jenerali Michael Luwongo Mstaafu
aliwataja wachezaji hao kuwa ni Nahodha Ayne Magombe, Sara Denis , Sophia
Mathius ,Hawa Wanyenche ,Christina Charles
na Angel Eaton huku mkuu wa Msafara akiwa ni Kapten Japhet Masai.
“ Nina matumaini makubwa na Kikosi hiki tunachokituma
Nigeria naamini kitarejesha furaha kwa Klabu ,jeshi na Watanzania kwa ujumla
ukizingatia uwezo Binafsi wa Wachezaji Mazoezi na Historia kutokana na michuano
iliyotangulia” Alisema Brigedia Jenerali Mstaafu Luwongo.
Kwa Upande wake mwenyekiti wa Chama cha Gofu nchini
TGU Joseph tango amelipongeza jeshi la Ulinzi la wananchi wa Tanzania kwa
jitihada katika kuendeleza michezo hasa mchezo wa gofu ambao klabu ya Lugalo
imekuwa kielelezo.
Aliomba mkuu wa majeshi ya ulinzi na Mlezi wa Klabu
ya Lugalo kuendelea kuisaidia Klabu hiyo ambayo ndio klabu yenye mashindano
mengi kwa mwaka ukilinganisha na Klabu nyingine nchini ikiwemo kusaidia utekelezaji
wa Ujenzi wa Uwanja makao makuu ya nchi Dodoma.
Mashindano
hayo ya Siku Tatu yanatarajiwa kuanza Tarehe Nane Februari huku
wachezaji kutoka nchi mbalimbali ikiwemo Kenya,Uganda, Zambia na
Malawi wakitarajiwa kushiriki.
No comments:
Post a Comment