HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

May 19, 2018

BENKI YA CRDB YASHIRIKI MAONYESHO YA WAJASIRIAMALI DAR

Meneja Biashara wa Benki ya CRDB, Tawi la Vijana, Zaituni Manora, akitoa sera za benki hiyo kwa wajasiriamali wa Manispaa ya Ilala, wakati wa ufunguzi wa maonyesho ya Wajasiriamali wa Manispaa ya Ilala na kufanyika katika Viwanja vya Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya maofisa wa Benki ya CRDB, wakiwa katika ufunguzi wa maonyesho ya wajasiriamali wa Manispaa ya Ilala, Viwanja vya Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya maofisa wa Benki ya CRDB, wakiandaa gari la kutolea huduma za kibenki katika ufunguzi wa maonesho ya wajasiriamali wa Manispaa ya Ilala, Viwanja vya Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salaam.
Ofisa Mikopo wa CRDB Bank, Josephat Shimo, akimwelekeza mmoja wa wananchi aliyefika kwenye banda la benki hiyo katika maonyesho hayo, jinsi ya kujaza fomu za miamala ya kifedha ya benki hiyo.
Baadhi ya maofisa wa Benki ya CRDB, wakiwa katika picha ya pamoja ndani ya banda lao tayari kwa kutoa huduma kwa wajasiriamali pamoja na wananchi uliojitokeza kwenye maonyesho hayo ya kazi za wajasiriamali.
Ofisa Mikopo wa Benki ya CRDB, Josephat Shimo, akiwapa maelezo baadhi ya wananchi waliofika kwenye banda la benki hiyo.
Ofisa Mikopo wa Benki ya CRDB, Josephat Shimo (kulia), akitoa maelezo kwa geni rasmi Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema, wakati wa ufunguzi wa maonyesho ya wajasiriamali wa Ilala.
Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema (kushoto), akimwuliza jambo Ofisa Mikopo wa Benki ya CRDB , Josephat Shimo (katikati), akiwa kwenye banda la benki hiyo, wakati akitembelea mabanda mbalimbali ya huduma za kifedha pamoja na ya wajasiriamali kabla ya kuyafungua maonesho hayo.  
Ofisa Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB, Makao Makuu, Richard Tangazo (kushoto), akimpa maelezo mmoja wa wajasiriamali aliyefika kwenye banda la benki hiyo katika maonyesho hayo.
Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema, akiwa meza kuu pamoja na baadhi ya Madiwani wa Manispaa ya Ilala kabla ya kuyafungua maonyesho hayo.
Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala, Omar Kumbilamoto, akizungumza wakati akimkaribisha mgeni rasmi, Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema kuzungumza katika ufunguzi wa maonesho hayo. 
Mgeni rasmi, Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema, akizungumza na wajasiriamali wa Manispaa ya Ilala, wakati akiyafungua maonyesho yao, viwanja vya Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salaam leo.
Mwenyekiti wa Kamati ya Huduma za Jamii, Diwani wa Gongolamboto, Jakob Kisi, akimkabidhi cheti cha kutambua mchango wa Benki ya CRDB, Meneja Biashara, Tawi la Vijana, Zaituni Manora, wakati wa ufunguzi wa maonesho hayo. Benki ya CRDB ilikuwa moja kati ya wadhamini katika maonyesho ya wajasiriamali Manispaa ya Ilala.
Ofisa wa Mikopo wa Benki ya CRDB, Josephat Shimo, akitoa maelezo kuhusu huduma mbalimbali zinazotolewa na benki hiyo kwa Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema. Katikati ni Meneja Mahusiano wa benki hiyo, Rachel Senni na kulia ni Zaituni Manoro.
Ofisa wa Benki ya CRDB, Julius Kessy, akitoa ufafanuzi kwa mteja wa benki hiyo aliyefika katika maonyesho ya wajasiriamali Wilaya ya Ilala na kudhaminiwa na benki hiyo.
Ofisa Mauzo wa Benki ya CRDB, Anifa Temba, akimuhudumia mteja wa benki hiyo aliyefika kufungua akaunti wakati wa maonyesho ya wajasiriamali.

No comments:

Post a Comment

Pages