May 11, 2018

MADIWA, WATENDAJI ZANZIBAR WATAKIWA KUWA MAKINI WAKATI WA KUPITISHA BAJETI

Na Talib Ussi
 
Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi, Ayoub Mohammed Mahmoud amewataka Madiwani na watendaji wa Manispaa ya Mjini kuzingatia shughuli zao za msingi wakati wakipitisha bajeti ikiwa ni pamoja utowaji wa huduma bora kwa jamii ya Zanzibar.

Ayoub alitoa wito huo wakati akifungua kikao cha bajeti ya makadirio na matumizi ya mwaka 2017-18 ya Baraza la Manispaa ya Mjini kilichofanyika katika ukumbi wa ofisi ya baraza hilo Malindi Mjini Unguja.

“Hivi sasa miundombinu katika maeneo mengi yameaza kuharibika, ni vyema mnapoandika bajeti yenu na hili mkaliangalia umuhimu mkubwa ili tuweze kuimarisha miundombinu yetu” alieelza Ayoub.

Alifahamisha kuwa madiwani ni wasimamizi wa shughuli ya baraza la manispaa hivyo ni vyema kusimamia na kutekeleza majukumu yao kikamilifu pamoja na kutathimini utekelezaji wa bajeti wanaziandaa ili kufikia hatua ya maendeleo sambamba katika kutimiza malengo ya baraza hilo katika kuwahudumia wananchi.

“Ikiwa tutapanga tuu bajeti ya kujiangalia katika bajeti iliyopita tulifikia maendeleo kwa kiasi gani , hatuwezi kufika kwa maana hiyo ni vyema kujitathimini” alitanabahisha Ayoub.

Aidha Mkuu wa Mkoa akizungumzia suala ukusanyaji wa mapato aliwahimiza wasimamizi hao kuzitizama vianzio mbaali mbali vya mapato vilivyomo katika manispaa hiyo hiyo ili kuona kianzio kipi cha mapato kinakusnya fedha nyingi ili kuiwekea bejeti kubwa ziweze kuongeza kukusanya mapato zaidi.

Ayoub alisisitiza kuwa bajeti itakayopangwa izingatie vipaumbele maalum vya baraza hilo ikiwa ni pamoja na kupabadilisha taswira na muonekano wa mji,uimarishaji wa miundombinu,usafi.

Aliongeza kuwa viongozi na watendaji wanawajibu mkubwa wa kutekeleza majumu yao kwa kuzingatia sheria,sera mbali mbali na miongozo ya nchi kama taratibu za serikali ya Mapinduzi Zanzibar katika kutoa huduma kwa jamii.

Mkuu wa Mkoa amewataka wadiwani hao kutoa mazingatio maalum katika utayarishaji wa bajeti hiyo kwenye sekta tofauti zilizogatuliwa ikiwemo Afya ya awali, elimu ya awali na msingi pamoja na kilimo katika kuzipa msukumo ili kuona zinatekelezwa kikamilifu. 

Akitoa shukrani kwa niaba ya viongozi na watendaji wa baraza hilo Diwani wa kuteuliwa Ali Juma Mohammed, aliahidi kutekeleza kwa vitendo maagizo na maelekezo waliyopewa ikiwa ni pamoja na kutoa mashirikiano yakutosha kwa watendaji wa baraza hilo sambamba na kuimarisha usafi wa mji na kutoa fursa ya kujiari kwa vijana.

No comments:

Post a Comment

Pages