May 02, 2018

Mkikita yatoa unga tani 1.7 Hocet

NA SULEIMAN MSUYA
MTANDAO wa Kijani Kibichi Tanzania (Mkikita), umetoa msaada wa unga wa muhogo tani 1.7 zenye thamani ya Sh. Mil 3.5 kwa Kituo cha Kulea watoto yatima Hananasifu (Hocet).
Msaada huo huo wa unga umekabidhiwa kwa Hocet na Mwenyekiti wa Bodi ya Mkiita, Dk. Kissui Kissui jana jijini Dar es Salaam.
Alisema wameamua kusaidia kituo hicho kama sehemu ya mchango wao kwa jamii na kwamba kiasi hicho ni sehemu ya mavuno ya kwanza ya uwekezaji wao katika kilimo hicho.
Dk. Kissui alisema Mkikita wamelima muhogo katika  maeneo ya Bagamoyo, Mkuranga na Kisarawe.“Tumelima muhogo katika mashamba yetu tumevuna na baada ya kusaga tumepata tani 15 hivyo tumekubaliana kutoa tani 1.7 Hocet ili vijana waweze kupata chakula kwa siku chache kwani ni wadau wetu,” alisema.
Mwenyekiti huyo alisema pamoja na msaada huo wa chakula kwa Hocet wanaamini kuwa kupitia wao watakuwa wamefikisha ujumbe kwa jamii kuhusu kufanya kilimo chenye tija zaidi.
Mkurugenzi wa Mkikita, Adam Ngamange alisema wametoa msaada huo kwa kituo cha watoto yatima wakiamini kuwa ni sehemu sahihi hata kwa maagizo ya Mungu.
“Mungu ameagiza yatima wasaidiwe na sisi katika mavuno yetu ya kwanza tangu kuanza kuwekeza wenyewe tumeona tuanze na vijana hawa ambao wanahitaji msaada na biashara itafuata,” alisema.
Ngamange aliwataka wakulima nchini kutumia Mkikita katika kutafua masoko ya bidhaa zao kwani uhakiki wa kupata soko ni mkubwa kutokana na mtandao waliona duniani.
Alisema Mkikita inajihusha na kilimo cha muhogo, papai, pilipili kichaa na mazao mengine ambayo yamekuwa yakihitajika katika nchi mbalimbali kama China, Uturuki na Ujerumani.
Mwanzilishi wa Hocet, Hezekia Mwalugaja, alisema msaada huo ni muhimu katika kituo chao na kwamba utataweza kusaidia changamoto ya chakula.
Mwalujaga alisema Mkikita imechagua sehemu sahihi katika kutoa msaada huo wa unga kwani ni dhahiri kituo kinahitaji na kuwataka wadau wengine kuinga mfano huo.
“Kimsingi hamjakosea kuja Hocet kwani tunawahitaji sana watu kama nyie lakini pia katika kituo tunafundisha masomo ya kilimo hivyo tunaenda pamoja kimtazamo na kupitia nafasi hii vijana watakuwa wamemahasika,” alisema.
Kwa upande wake Hamida Shaaban, mmoja wa watoto katika kituo hicho alisema msaada huo umesababisha watambue kuwa wapo watu wanaowajali kutokana na hali zao.

No comments:

Post a Comment

Pages