May 02, 2018

NGORONGORO HEROES KUWAKARIBISHA MALI MEI 13,MASHABIKI KUIONA KWA KIINGILIO CHA ELFU 1

Timu ya Taifa ya Vijana chini ya miaka 20 (Ngorongoro Heroes) itacheza na timu ya Taifa ya Mali U20 Jumapili Mei 13,2018 Uwanja wa Taifa Dar es Salaam.

Katika mchezo huo utakaochezwa saa 10 jioni kiingilio cha kuingia Uwanjani kutazama mechi hiyo VIP zote shilingi 3,000 Mzunguko shilingi 1,000.
Ngorongoro Heroes wapo kambini wakiendelea kujiandaa na mchezo huo,leo wapo kwenye ratiba ya kufanya mazoezi ya gym asubuhi na jioni kabla ya kuwa na mazoezi ya uwanjani kesho na Ijumaa ambapo kesho Alhamisi watakuwa na kipindi kimoja cha Uwanjani saa 10 kwenye Uwanja wa Uhuru wakati Ijumaa watafanya vipindi viwili asubuhi na jioni saa 10.
Kikosi hicho hakina majeruhi vijana wana morali kubwa ya kufanya vizuri katika mchezo huo wa kwanza wa raundi ya pili ya kufuzu fainali za vijana Africa.
LIGI YA MABINGWA WA MIKOA KUANZA KUTIMUA VUMBI MEI 6,2018
Ligi ya Mabingwa wa Mikoa(RCL) inatarajia kuanza kutimua vumbi kuanzia Jumapili Mei 6 na kumalizika Mei 22,2018 kwenye vituo vinne.
Ligi hiyo ya RCL itashirikisha timu 28 zilizogawanywa kwenye makundi manne kwenye vituo vya Geita,Singida,Rukwa na Kilimanjaro na kila kundi kwenye kituo likiwa na timu 7.
Kila kundi litapandisha timu 2 wakati zitakazobaki zitarudi ligi ya mkoa.
IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA TFF

No comments:

Post a Comment

Pages