Na Mwandishi Wetu
Nahodha wa timu ya soka ya taifa ya Tanzania (Taifa Stars), Mbwana Samatta anayecheza soka lake nchini Ubeligiji katika klabu ya KRC Genk, Mbwana Samatta ameipongeza kampuni ya kuuza maziwa ya Asas Dairies kwa kujitokeza kudhamini kampeni yake ya “Nifuate”.
Kampeni hiyo ilikutanisha timu mbili, timu Samatta na timu-Kiba ambazo ziliwajumuisha mastaa wengine wengi wa soka la Tanzania, muziki na waigizaji.
Aizungumza jijini, Samatta alisema kuwa wazo la kuanzisha kampeni hiyo alilichukulia kama utani tu, lakini kampuni hiyo na wadau wengine wameamua kuunga mkono na kuwa suala la Kitaifa.
Samatta alisema kuwa kampuni hiyo na wadau wengine wameonyesha jinsi gani wanavyojali maslahi ya Taifa na kuahidi kushirikiana nayo katika kampeni nyingine mbalimbali.
“Kwa kweli nawashukuru wadhamini kwa sapoti yao kubwa katika kampeni hii ambayo lengo lake kubwa ni kutatua changamoto za elimu nchini, huu ni mwanzo tu, kwani natarajia kufanya mambo mengine makubwa kwa jamii hapo baadaye,” alisema Samatta.
Alisema kuwa anatarajia kupata mafanikio makubwa katika kampeni hiyo ambayo ilifanyika kwa mara ya kwanza katika historia.
“Lengo si kupata fedha, lengo ni kuchangia na tupo tayari kupokea chochote kutoka kwa wadau ambacho kitaisaidia maendeleo ya elimu hapa nchini. Tutaendelea kupokea misaada hata baada ya mechi,” alisema.
No comments:
Post a Comment