Mchezaji wa Kimataifa, Mbwana Samata, akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam jana kuhusu mechi maalumu ya timu Samata na Alikiba ya kujitolea kwa ajili ya kuchangia elimu. Kuliani Msanii wa vichekesho, Lucas Mhavile 'Joti'.
Na Mwandishi Wetu
MWANASOKA wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Samatta anayekipiga katika klabu ya KRC Genk ya Ubelgiji na msanii maarufu, Ali Kiba, wanatarajia kuoneshana kazi katika mechi ya hisani ya soka kwa ajili ya kuchangia elimu hapa nchini itakayofanyika Julai 9, 2018.
Mechi hiyo itakayochezwa usiku wa leo katika uwanja wa Taifa jijini, Dar es Salaam, unalenga kupata fedha za kusaidia sekta ya elimu hapa nchini kama sehemu ya kurejesha shukrani kwa jamii.
Mechi hiyo itakayochezwa usiku wa leo katika uwanja wa Taifa jijini, Dar es Salaam, unalenga kupata fedha za kusaidia sekta ya elimu hapa nchini kama sehemu ya kurejesha shukrani kwa jamii.
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana katika mkutano uliofanyika uwanja wa Taifa, Samatta alisema maandalizi yamekamilika na kuwaomba wapenzi na mashabiki kujitokeza kwa wingi.
Alisema mechi hiyo maalumu kwa ajili ya kusaidia jamii, inalenga kupata kiasi cha shilingi mil.50, hivyo mashabiki wa soka na muziki wajione ni mechi yao.
Samatta alisema mbali ya kutafuta fedha hizo na kutoa burudani, mechi hiyo inalenga kuhimiza umoja na ushirikiano baina ya vijana katika masuala ya kiuchumi na kijamii.
Alisema ingawa wameanzia katika sekta ya elimu katika kusaidiana na serikali kukabili changamoto zilizopo, wakati mwingine watajielekeza kwingineko.
“Wazo la mchezo kati yangu na Kiba nililifikiria kiutani, kwa sababu niliwahi kuona Kiba akicheza soka. Nilitamani tucheze mechi ambayo itatengeneza urafiki zaidi ambako wazo limetanuka zaidi na kuelekezwa kwenye elimu,” alisema Samatta.
Kocha wa timu ya Samatta Jamhuri Kiwhelu ‘Julio’ alisema, wameamua kujikita kuchangia elimu kwa sababu Rais John Magufuli ameonesha kuelekeza nguvu zake katika eneo hilo kwa kutoa elimu bure.
Julio alisema wao wameona ni bora kuungana na rais kuchangia elimu ambayo ambaye akiona kuna wanaomsapoti kwa baadhi ya mambo atafarijika.
Kuhusu kikosi chake kiko katika hali nzuri kwani ana kikosi chenye wachezaji bora hatoumiza kichwa kwa sababu ya kujitambua kwa wachezaji hao.
“Kikosi changu kina wachezaji wenye kujitambua, sitopata tabu kutoa maelekezo kwani wote wako vizuri katika mchezo.
Msemaji wa timu hiyo, Lucas Mhuvile ‘Joti’ alisema wamejipanga kuonesha kandanda safi katika mchezo huo, hivyo timu Kiba wajiandae kupokea kipigo katika mchezo huo.
Joti alisema kwa kuanzia wameanzia kwenye elimu hivyo watapanua wigo wa kutekeleza majukumu ya jamii ambayo yanahitaji msaada wa jamii.
Mratibu wa mechi hiyo, Hussein Hembe alisema fedha zitakazopatikana kupitia viingilio hizo zitatumika kwa ajili ya kununulia vifaa vya elimu kama vile vitabu na kompyuta.
“Niwaombe tu Watanzania wenzetu mabibi na mabwana kujitokeza kwa wingi siku hiyo uwanjani kwa ajili ya kuja kuwaunga mkono Samatta na Kiba katika kufanikisha jambo hilo,” alisema Hembe.
Kwenye kikosi hiko Samatta amewataja mastaa wa zamani na sasa hivi kwenye soka hapa nchini pamoja na mchezaji mahiri wa TP Mazembe, Trésor Mputu, huku wachezaji waliotajwa kwenye kikosi hiko ni Juma Kaseja, Kabaly Faraji, Shomari Kapombe, Mohammed Zimbwe, Kelvin Yondani, Nadri Haroub, Athumani Chuji, Haruna Shamte, Mohammed Samatta, Thomas Ulimwngu, Farid Musa, Haruna Boban na Amri Kiemba.
Wengine ni Athumani Machupa, Henry Joseph, Rashid Gumbo, Mrisho Ngasa, Sultan Kaskas, Saleh Jembe na Shaffih Dauda.
Huku kikosi cha Kiba kinaundwa na Shaban Kado, Aishi Manula, Gadiel Michael, Said Ndemla, Adam Salamba, Paul Nonga, Abdu Kiba, Himid Mao, Erasto Nyoni, Aggrey Morris, Ibrahim Ajib, Haruna Niyonzima, Abdi Kassim, Emmanuel Okwi, Abdi Banda, Simon Msuva, Shaban Kisiga, Uhuru Selemani na Ramadhani Chombo.
No comments:
Post a Comment