Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Jenista Mhagama, akizungumza na waandishi wa habari alipokutana nao hii leo Jijini Dodoma.
Na Mpiga Picha Wetu).
Waziri Mhagama ametengua
Bodi ya Shirika la Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF). Utenguzi huo
umeanza hii leo tarehe 24 Julai, 2018, baada ya hatua mbalimbali za Serikali ya
Awamu ya Tano kuendelea kuimarisha utendaji kazi wa Taasisi na Mashirika yake.
Hayo yamesemwa na Waziri wa
Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu)
Mhe.Jenista Mhagama (MB) alipokutana na waandishi wa habari hii leo Mjini
Dodoma Julai 24, 2018.
Waziri Mhagama alieleza
kuwa, kwa mujibu wa mamlaka aliyonayo kama Waziri wenye dhamana kwenye masuala
ya hifadhi ya jamii ninatangaza rasmi kuivunja Bodi ya Wadhamini wa Mfuko wa
Taifa wa Hifadhi ya Jamii pamoja na uteuzi wa Wajumbe wote wa bodi hiyo.
“Lengo kuu la madiliko haya
ni kuhakikisha kuwa shirika hilo linaimarishwa zaidi sambamba na kusimamia
mwenendo wa kila siku wa shirika ikiwemo zile kazi za msingi kuongeza wanachama,
kukusanya michango, kulipa mafao kwa wakati na kusimamia vitega uchumi kwa
uzalendo na weledi” alisisitiza Mhagama
Aidha, Waziri Mhagama alitoa
taarifa rasmi kuhusu mfumo utakao tumika kuadhimisha siku ya kumbukumbu ya
Mashujaa ambayo hufanyika tarehe 25 Julai kila mwaka. Katika kutekeleza agizo
la Mhe. Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, fedha zilizopangwa kufanyia
maandalizi ya sherehe hizo Kitaifa ambazo ilikuwa zifanyike kwenye Jiji la
Dodoma zitatumika kuboresha miundombinu ya barabara katika Jiji la Dodoma.
“Mwaka huu 2018 hakutakuwa
na maadhimisho ya pamoja ya siku ya kumbukumbu ya mashujaa, baadala yake kila
Mkoa, Wilaya, Kata na Vijiji watafanya maadhimisho ya siku hiyo kwa kufanya
usafi katika maeneo waliyozikwa Mashujaa wetu na maeneo yoyote ambayo
yanakumbukumbu za Mashujaa wetu nchini” Alisema Mhagama.
HABARI/PICHA KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKANI OFISI
YA WAZIRI MKUU KAZI, VIJANA, AJIRA NA MWENYE ULEMAVU
No comments:
Post a Comment