HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

August 20, 2018

CMSA,CISI Kuendesha Mafunzo ya Kitaaluma


Kaimu Ofisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA), Nicodemus Mkama, akitoa hotuba yake wakati uzinduzi wa Mpango wa Mafunzo Endelevu ya Kitaaluma kwa Watendaji katika Masoko ya Mitaji Tanzania. (Picha na Francis Dande).

Mkurugenzi wa Global Business Development of Chartered Institute For Securities and Investment (CISI), Kevin Moore, akitoa mada wakati uzinduzi wa Mpango wa Mafunzo Endelevu ya Kitaaluma kwa Watendaji katika Masoko ya Mitaji Tanzania.

Baadhi ya washiriki.

Washiriki wa mafunzo.

Mwakilishi kutoka Chama cha Madalali wa Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE), Arphaxad Masambu, akizungumza katika uzinduzi huo.

Christian Mpalazi kutoka FSDT, akizungumza
wakati uzinduzi wa Mpango wa Mafunzo Endelevu ya Kitaaluma kwa Watendaji katika Masoko ya Mitaji Tanzania.
Baadhi ya washiriki.

Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Wakurugenzi ya CMSA, Emmanuel Kakwezi, akizundua rasmi Mpango wa Mafunzo Endelevu ya Kitaaluma kwa Watendaji katika Masoko ya Mitaji Tanzania.

Tunajifunza.

Mafunzo yakiendelea.

Picha ya pamoja.


NA MWANDISHI WETU

MAMLAKA ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA) na Taasisi ya Mafunzo ya Masoko ya Mitaji na Uwekezaji ya nchini Uingereza (CISI) zimezindua mpango wa kuendesha mafunzo endelevu ya kitaalamu kwa washiriki wa masoko ya mitaji(CPD) nchini.

Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Kaimu Mtendaji Mkuu wa CMSA, Nicodemus Mkama, alisema kwamba mpango huo unaweka utaratibu na vigezo vya ushiriki kwa washirika wa masoko ya mitaji kufikia angalau saa kumi ya mafunzo kwa mwaka.

Mkama alisema hatua hiyo ni kutokana na kigezo cha cha utoaji leseni ya ushiriki katika masoko ya mitaji ifikapo Januari 2020.

“Washiriki wa masoko ya mitaji walio na leseni watatakiwa kufanya mafunzo na kutekeleza mipango inayotambuliwa na CMSA na CISI katika utekelezaji vigezo vya mpango wa mafunzo endelevu na kulewa idhini itakayotolewa kwa taarifa maalumu iliyowasilishwa na CMSA kwaajili ya taarifa,”alisema

Aidha alisema kwamba CPD utawawezesha watendaji ndani ya masoko ya mitaji kutoa huduma kwa umahiri na kuendana na maendeleo yanayotokea katika masoko ya mitaji duniani.

Mkama alisema mpango wa mafunzo endelevu unahusisha kufuatilia kwa ukaribu na kuweka kumbukumbu ya maarifa, ujuzi na uzoefu ambayo mtu hupata katika utendaji kazi ndani ya masoko.

“Ushirikiano kati ya CMSA na CISI unayaweka masoko ya mitaji ya Tanzania katika ramani ya masoko ya mitaji ya dunia kwa kuwa na wataalamwanaokidhi viwango vya kimataifa,”alisema.

Mgeni rasmi, Mjumbe wa bodi ya wakurugenzi wa CMSA, Emmanuel Kakwezi, alisema masoko ya mitaji ni sekta inayobadilika kwa kasi na yenye kuhusisha viashiria vya aina mbalimbali hivyo ni muhimu kwa watendaji wa ndani ya masoko kuwa na uwezo wa kufahamu mambo yanayoendelea duniani.

Aidha aliitaka CMSA kuhakikisha wataalamu wote wa masoko ya mitaji wanajiunga na mpango huo ili kulinda uwezo wa kutaalamu na uhalali wao katika ulimwengu wa ushindani.

No comments:

Post a Comment

Pages