WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa amesema Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya
Makazi, William Lukuvi atakwenda katika Halmashauri ya Manispaa ya
Tabora ili kutatua kero kubwa za ardhi.
PMO 0883 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiteta na Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Tabora, Munde Tambwe katika mkutano wa hadhara aliouhutubia kwenye kiwanja cha chipukizi katika Manispaa ya Tabora.
Wananchi wa Manispaa ya Tabora wakimsikiliza Waziri Mkuuu, Kassim Majaliwa wakati alipohutubia mkutano wa hadhara kwenye kiwanja cha Chipukizi.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akisalimiana na Mbunge wa zamani wa Tabora Mjini, Aden Rage baada ya kuhutubia mkutano wa hadhara katika kiwanja cha Chipukizi kwenye Manispaa ya Tabora, Agosti 18, 2018. Katikati ni Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanri.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Tabora, Kamishina Msaidizi wa Polisi, Emmanuel Nley jumla ya shilingi 1,500,000/= kwa ajili ya ujenzi wa dawati la Jinsia katika Mji wa Tabora na ujenzi wa nyumba ya Mkuu wa polisi katika wilaya ya Igunga. Makabidhiano ya fedha hizo zilizotolewa na Mbunge wa Manonga, Seif Khamis Gulamali (kushoto) yalifanyika baada ya Waziri Mkuu kuhutubiua mkutano wa hadhara katika kiwanja cha Chipukizi kwenye Manispaa ya Tabora, Agosti 18, 2018. Wapili kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanri na wapili kushotoi ni Mbunge wa Viti Maalum, Munde Tambwe.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akihutubia mkutano wa hadhara kwenye kiwanja cha Chipukizi katika Manispaa ya Tabora, Agosti 18, 2018. (Picha zote na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Ameyasema
hayo jana jioni (Jumamosi, Agosti 18 ,2018) wakati akizungumza na
wananchi wa Manispaa hiyo katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye
Uwanja wa Chipukizi.
Waziri
Mkuu aliyasema hayo baada ya wabunge na wananchi kueleza changamoto
kubwa zinazowakabili ikiwe ya migogoro ya ardhi iliyodumu kwa muda
mrefu.
“Waziri
wa Ardhi atakuja hapa na ramani zake, atakutana na watendaji na
kumaliza matatizo yote makubwa ya ardhi na yale madogo madogo
yatashughulikiwa na Mkuu wa Wilaya,”.
Katika hatua nyingine,Waziri
Mkuu alisema wilaya zote zinatakiwa zihakikishe zinakuwa na shule moja
ya kidato cha tano na sita kwenye kila tarafa nchini na Serikali
itapeleka walimu.
Alisema
uwepo wa shule hizo utaamsha ari ya wanafunzi kusoma kwa bidii, jambo
litakaloongeza idadi ya wanaoendelea na masomo ya kidato cha tano na
sita.
Kadhalika
Waziri Mkuu aliwaagiza watendaji wote kuanzia ngazi ya halmashauri hadi
vijiji wawasimamie wanafunzi wa kike na wahakikishe wanamaliza masomo
bila ya kukatishwa.
“Huu
ni mkakati wa Taifa tunataka watoto wa kike wote walindwe ili waweze
kumaliza shule na marufuku kukatisha elimu yao, iwe kwa kuwapa ujauzito
au kuwaoa, adhabu yake ni kali,”.
Waziri
Mkuu jana jioni alimaliza ziara yake ya kikazi ya siku tatu mkoani
Tabora baada ya kuwa amefanya ziara katika wilaya za Igunga, Nzega na
Halmashauri ya Manispaa ya Tabora.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMAPILI, AGOSTI 19, 2018.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiteta na Mwenyekiti wa CCM wa mkoa wa
Tabora, Hassan Kasubi katika mkutano wa hadhara aliouhutubia kwenye
kiwanja cha Chipukizi katika Manispaa ya Tabora, Agosti 18, 2018. PMO 0883 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiteta na Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Tabora, Munde Tambwe katika mkutano wa hadhara aliouhutubia kwenye kiwanja cha chipukizi katika Manispaa ya Tabora.
Wananchi wa Manispaa ya Tabora wakimsikiliza Waziri Mkuuu, Kassim Majaliwa wakati alipohutubia mkutano wa hadhara kwenye kiwanja cha Chipukizi.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akisalimiana na Mbunge wa zamani wa Tabora Mjini, Aden Rage baada ya kuhutubia mkutano wa hadhara katika kiwanja cha Chipukizi kwenye Manispaa ya Tabora, Agosti 18, 2018. Katikati ni Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanri.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Tabora, Kamishina Msaidizi wa Polisi, Emmanuel Nley jumla ya shilingi 1,500,000/= kwa ajili ya ujenzi wa dawati la Jinsia katika Mji wa Tabora na ujenzi wa nyumba ya Mkuu wa polisi katika wilaya ya Igunga. Makabidhiano ya fedha hizo zilizotolewa na Mbunge wa Manonga, Seif Khamis Gulamali (kushoto) yalifanyika baada ya Waziri Mkuu kuhutubiua mkutano wa hadhara katika kiwanja cha Chipukizi kwenye Manispaa ya Tabora, Agosti 18, 2018. Wapili kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanri na wapili kushotoi ni Mbunge wa Viti Maalum, Munde Tambwe.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akihutubia mkutano wa hadhara kwenye kiwanja cha Chipukizi katika Manispaa ya Tabora, Agosti 18, 2018. (Picha zote na Ofisi ya Waziri Mkuu)
No comments:
Post a Comment