Bendi maarufu ya Muziki wa dansi barani ulaya
The Ngoma Africa Band aka FFU-Ughaibuni ukipenda waite viumbe wa ajabu
Anunnaki au "Watoto wa Mbwa" inayoongozwa na kamanda Ras Makunja
inatarajiwa kulitingisha jukwaa la Alafia Festival katikani ya jiji la
Hamburg katika viwanja vya hamburg-Altona Ujerumani siku ijumaa tarehe
24-08-2018 kuanzia majira ya saa 2.00 usiku (20.00 hour), bendi hiyo
maarufu inayodumu kwa miaka 24 katika majukwaa ya kimataifa na mtindo
wake wa "Bongo Dansi" made in Uswahilini inazidi kuwanasa washabiki
katika kila pembe barani ulaya,ni juzi kati tu ilitumbuiza katika
onyesho kubwa mjini Tuebingen, Ujermani na Mamling Festival nchi
Austria,na ijumaa ya tarehe 24 Augosti 2018 watatingisha tena mjini
Hamburg-Altona.usikose kuungana nao katika tamasha hilo la wazi pia
unaweza jumuika nao at www.facebook.com/ngomaafricaba nd au www.ngoma-africa.com
Bendi maarufu barani ulaya Ngoma Africa band wakifanya yao kimataifa.
Kamanda Ras Makunja wa Ngoma Africa Band.
Ngoma Africa band.
Ngoma Africa Band aka FFU.
No comments:
Post a Comment