Wateja wa Halotel sasa kutuma pesa bure
Naibu Mkurugenzi wa Kampuni ya Halotel, Nguyen
Van So, akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa kampeni ya “Ninogeshe na Halopesa” maalum kwa wateja wanaotumia huduma za Halopesa ambapo wateja wa Halopesa wataweza kutuma pesa bure Halopesa kwenda Halopesa muda wowote.
Mkuu wa Kitengo
cha Mawasiliano wa Halotel, Mhina Semwenda, akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa kampeni ya 'Ninogeshe na Halopesa'
Msanii wa muziki wa kizazi kipya ambaye pia ni Balozi wa Halotel, Faustina Mfinanag 'Nandi', akizungumza na waandishi wakati wa hafla ya uzinduzi wa kampeni ya 'Ninogeshe na Halopesa'
Balozi wa Halotel, Faustina Mfinanag 'Nandi', akiimba kibao chake maalumu kwa ajili ya kampeni ya 'Ninogeshe na Halopesa'
Na Mwandishi Wetu
Kampuni ya Mawasiliano ya Halotel imezindua kampeni kabambe ya “Ninogeshe na Halopesa” maalum kwa wateja wanaotumia huduma za Halopesa.
Kuanzia sasa, wateja wa Halopesa wataweza kutuma pesa bure Halopesa kwenda Halopesa muda wowote.
Kuzinduliwa
kwa kampeni hiyo ni muendelezo wa azma ya kuboresha huduma za fedha kwa
njia ya mtandao kwa wananchi wenye vipato tofauti.
Licha
ya kuondoa gharama za miamala kwa wateja wanaotuma fedha kutoka Halotel
kwenda Halotel, wateja wetu watapata nafuu wanapotuma fedha kutoka
Halopesa kwenda mitandao mingine.
Kampeni
hii ni maalum kwa wateja wote wa Halotel waliopo mjini na vijijini
wanaotumia huduma zetu kwa miaka miwili sasa tangu tulipoingia sokoni
ambao watanufaika zaidi kwa kuokoa fedha ambazo wangekatwa wanapotuma
pesa. Fedha hizo sasa wataweza kuzitumia kukidhi mahitaji yao mengine.
Akizungumza
na waandishi wa habari, Naibu Mkurugenzi wa Kampuni ya Halotel, Nguyen
Van Son amesema kampeni hii ni hatua nyingine ya kuhakikisha wateja
wanakuwa na wigo mkubwa kufurahia na kunufaika zaidi na huduma za
Halopesa bila kuwa na wasiwasi wa makato kila wanapotuma pesa mahali
popote na wakati wowote.
“Hii
ni fursa nyingine kwetu kuongeza tabasamu na furaha kwa wateja wetu
walioenea nchi nzima kwa kuwapa huduma za fedha iliyo madhubuti
inayoendana na hali ya uchumi kuondokana na usumbufu ambao wangeupata
kwa kutumia njia nyingine kutuma fedha. Sasa wataokoa makato ya kufanya
miamala,” alisema Son.
Mkurugenzi
huyo alibainisha kwamba licha ya kuondoa gharama katika kutuma fedha
kutoka Halopesa kwenda Halopesa, wateja watapata muda wa maongezi bure
kila wanapoweka pesa kwa wakala.
“Habari
njema tuliyonayo kwa wateja wetu ni kuendelea kuwanufaisha kila
wanapotumia huduma ya Halopesa ambapo kwa sasa kila mteja atakaye weka
pesa kwa wakala kuanzia shilingi elfu moja (1,000/=) atapata muda wa
maongezi wa bure. Si hivyo tu wateja wetu wataendelea kunufaika kwa
namna mbalimbali kila wanapotumia huduma za Halopesa,” alihitimisha Son.
Sambamba na uzinduzi wa kampeni ya Ninogeshe na
Halopesa, kampuni ya Halotel imeingia makubaliano na msanii chipukizi
wa kike wa nyimbo za kizazi kipya (bongo fleva), Faustina Mfinanaga
maarufu kama “Nandi” kuwa balozi wake ambaye atahusika katika kampeni za
Halopesa.
Hii
ni hatua nyingine kwa msanii huyu kufanyakazi na Halotel na kuwakilisha
huduma bora za mawasiliano inayotoa kwa mamilioni ya Watanzania nchi
nzima.
Akizungumza
katika hafla fupi ya kusaini mkataba na msanii huyo, Mkuu wa Kitengo
cha Mawasiliano wa Halotel, Mhina Semwenda amesema kampuni imemchagua
Nandi kwa sababu ana uwezo wa kuwa na mchango chanya utakaosaidia kukuza
mauzo ya bidhaa na huduma, pamoja na kuimarisha jina la kampuni.
“Nandi
ni msanii anayekonga nyoyo za mashabiki wake kupitia wimbo wake
unaovuma kwa jina la ‘Ninogeshe’ na kumpa umaarufu unamfanya afahamike
kwa watu wa rika zote. Unampa umaarufu ambao utasaidia kuiwakilisha vema
kampuni ya Halotel,” alisema Semwenda.
Kwa
upande wake, msanii wa bongofleva, Faustina Mfinanga (Nandi) amesema
hiyo ni fursa kubwa na ya kipekee kwake kuwa miongoni mwa familia ya
kampuni hiyo na kupewa jukumu la kuiwakilisha ipasavyo kwa wateja wake
na watanzania kwa ujumla kutokana na huduma bora za mawasiliano
inazotoa.
Huduma ya Halopesa inatolewa na zaidi ya mawakala 55,000 wanawahudumia zaidi ya wateja milioni 1.5 walioenea nchi nzima.
No comments:
Post a Comment