Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali
Mohamed Shein (kushoto) akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja
Mhe.Hassan Khatib Hassan wakati alipowasili katika Uwanja wa Jamhuri
Makunduchi Wilaya ya Kusini Unguja leo kabla ya Swala ya Eid el
Hajj,Kitaifa iliyoswaliwa katika Mkoa wa Kusini Unguja ambapo waislamu
mbali mbali walihudhuria. (Picha na Ikulu).
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk. Ali
Mohamed Shein (katikati) akisalimiana na Mashekhe wakati alipowasili
katika Uwanja wa Jamhuri Makunduchi Wilaya ya Kusini Unguja kabla ya
Swala ya Eid el Hajj,Kitaifa iliyoswaliwa katika Mkoa wa Kusini Unguja
ambapo waislamu mbali mbali katika Mkoa huo walihudhuria.
Waislamu
mbalimbali wa Mkoa wa Kusini Unguja wakiwa katika swala ya Eid el
Hajj,Kitaifa iliyoswaliwa leo katika Uwanja wa Jamhuri Makunduchi
Wilaya ya Kusini,ambapo Sheikh Suleiman Haji Ibrahim(hayupo pichani)
aliongoza Swala hiyo,iliyohudhuriwa na Viongozi wa Kitaifa akiwemo Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk. Ali Mohamed Shein.
Baadhi ya akinamama waliojumuika katika swala ya Eid el Hajj,Kitaifa iliyoswaliwa leo katika Uwanja wa Jamhuri Makunduchi Wilaya ya Kusini, Mkoa wa Kusini Unguja.
Baadhi ya viongozi na wananchi waliohudhuria Swala ya Eid el Hajj wakisikiliza hotuba iliyosomwa na Sheikh Abdalla Issa Makame (hayupo pichani) kutoka Kijiji cha Paje Wilaya ya Kusini, ambapo viongozi wa kitaifa walihudhuria katika Swala hiyo iliyoswaliwa Kitaifa katika Uwanja wa Jamhuri Makunduchi Mkoa wa Kusini Unguja.


No comments:
Post a Comment