Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa
Umma na Utawala Bora, Kapt. (Mst)
Mhe. George H. Mkuchika (Mb) akiwasili katika Chuo cha Taifa cha Ulinzi, jijini
Dar es Salaam kufunga kozi ya siku tano ya viongozi.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa
Umma na Utawala Bora, Kapt. (Mst)
Mhe. George H. Mkuchika (Mb) akimtunuku cheti Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto
James baada ya kuhitimu kozi fupi ya tano ya Viongozi iliyofanyika katika Chuo cha Taifa
cha Ulinzi, jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa
Umma na Utawala Bora, Kapt. (Mst) Mhe.
George H. Mkuchika (Mb) akizungumza na washiriki wa kozi fupi ya tano ya
Viongozi, iliyofanyika katika Chuo cha Taifa cha Ulinzi, jijini Dar es
Salaam.
Mkuu wa Mkoa wa
Kilimanjaro, Mhe. Anna Mghwira akitoa neno la shukrani baada ya kuhitimu kozi fupi ya tano ya Viongozi katika Chuo cha Taifa
cha Ulinzi, jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na
Utawala Bora, Kapt. (Mst) Mhe. George
H. Mkuchika (Mb) akipokea zawadi ya tai, kutoka kwa Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Ulinzi
(NDC) Luteni Jenerali, Paul Massao, baada ya kufungua kozi fupi ya tano ya
Viongozi, iliyofanyika katika Chuo cha Taifa cha Ulinzi,
jijini Dar es Salaam.
Viongozi na Watumishi
nchini wamekumbushwa kutanguliza mbele moyo wa uzalendo na masilahi mapana ya
taifa wanapotekeleza majukumu yao ili kupeleka maendeleo ya taifa mbele na
kuimarisha usalama wa taifa.
Hayo yamesemwa na Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt (Mst) Mhe. George
H. Mkuchika (Mb) wakati akifunga kozi fupi ya tano kwa viongozi iliyofanyika
Chuo cha cha Taifa cha Ulinzi - Tanzania (NDC) jijini Dar es Salaam.
Mhe. Mkuchika
amesema, ni matumaini kuwa washiriki waliohudhuria kozi hiyo, utendaji wao wa
kazi utabadilika kwa kuwa na tija kwani sasa mbinu zote zinazohusu namna ya
kufikiri kimkakati, kufanya tathmini katika mambo mbalimbali ili kufikia
maamuzi wamezipata.
“Sasa mnatambua
dhana ya usalama wa Taifa vema na kwa mapana zaidi, si kulinda mipaka na mali
za wanajamii tu, bali pia inahusisha kutunza mazingira, kuwa na chakula cha
kutosha, kupiga vita rushwa na madawa ya kulevya na mengine mengi ambayo ninyi
mnayafahamu zaidi,” Mhe. Mkuchika amesema na kuongeza kuwa usalama wa watu ni
muhimu kuliko jambo jingine lolote, hivyo masuala ya usalama yawe ni sehemu ya
kuzingatia katika utendaji wa kila siku na hasa pale maamuzi yanayogusa masilahi
ya nchi na jamii yanapotolewa.
Aidha, Mhe.
Mkuchika amesema, Serikali ya Awamu ya Tano chini ya uongozi wa Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli imedhamiria kwa dhati
kuipeleka nchi katika Uchumi wa Viwanda, lakini suala la rushwa limekuwa kikwazo
kikubwa kufikia lengo hilo, hivyo ni jukumu la viongozi wote kutoa majawabu ya
namna gani malengo yatafikiwa.
Kwa upande wake, Mkuu
wa Chuo cha Taifa cha Ulinzi -Tanzania, Luteni Jenerali Paul Massao ameishukuru
Serikali kwa kuhakikisha viongozi na watumishi wengine wanahudhuria kozi hiyo
muhimu kwa masilahi ya taifa.
Jumla ya wahitimu
24 walikabidhiwa vyeti, baadhi yao wakiwa ni Waheshimiwa Naibu Mawaziri, Makatibu
Wakuu, Waheshimiwa Wakuu wa Mikoa, Viongozi wa vyombo vya Ulinzi na Usalama,
Viongozi Waandamizi wa Taasisi za Serikali.
Mtaala wa kozi hiyo
ulilenga katika masuala yanayohusu masilahi, uzalendo na dhana nzima ya usalama
wa taifa.
IMETOLEWA NA:
KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI
OFISI YA RAIS (UTUMISHI)
TAREHE 18 AGOSTI,
2018
No comments:
Post a Comment