HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

September 13, 2018

Ngoma Africa Band na muzimu wao wa Muziki wa Bongo Dansi umewaganda Ulaya!

 Ngoma Africa band kibaruani.
Ngoma Africa Band wakiwa jukwaani barani  ulaya. 
Mkuu Kamanda Ras Makunja.
 Aj Nbongo mpiga bass guitar wa ngoma  Africa Band.
 Chris-B mwimbaji na mpiga solo guitar  wa Ngoma Africa band.
 Jessica Ouyah dansa pia mwimbaji wa  kike wa Ngoma Africa Band.
 Jojo Zuza mpiga drum chipukizi wa Ngoma  Africa Band.

 Vially Nbongo mpiga Rhythm wa Ngoma  Africa Band.

  Mshike mkamate ya kina Ras Makunja na  washabiki.

 Wapenzi wa Muziki wa Ngoma Africa Band  wakipata burudani ya bendi hiyo.
 Princess Florette Pedro mwimbaji wa  kike chipukizi wa Ngoma Africa Band.

Na Zainabu Ally Khamis

Ngoma Africa Band na muzimu wao wa Muziki wa Bongo Dansi umewaganda Ulaya! Unapotaja muziki wa dansi la kiafrika katika tufe la dunia bendi maarufu ya muziki wa dansi barani ulaya "The Ngoma Africa Band" aka FFU-Ughaibuni au Viumbe wa ajabu "Anunnaki Aliens yenye makao yake nchini ujerumani uwezi kukosa kuitaja bendi hiyo inayodumu kwa miaka 25 toka kuanzishwa kwake na kiongozi wake mtanzania Ebrahim Makunja aka Kamanda Ras Makunja.

 
Bendi hiyo na muziki wake wa dansi au "Bongo Dansi" made in Uswahilini ndio bendi pekee iliyofanikiwa kuwanasana washabiki katika kila pembe barani ulaya kwa kutumia ulimbo wa mdundo wake wa "Muziki wa Dansi" ambao kwa nyumbani Tanzania unaonekana kama unachimbiwa kaburi kwa makusudi lakini kimataifa Ras Makunja na kikosi chake cha Ngoma Africa Band kinapeperusha bendera majukwaani na muziko huo wa dansi kugeuka jinamizi kubwa liliwakaa moyoni na vichwani mashabiki hao wa kimataifa. 

ni hivi juzi kati tu katika msimu wa joto barani ulaya Ngoma Africa band imefanikiwa kutingisha majukwaa makubwa ya Mamling (Austria),Tallinn(Estonia), majukwaa makubwa ya UjerumaniBrinkenreid Festival,Regensburg Festival,GaiExpo Tubingen na juzi tu Alafia Festival Hamburg yote yalifunikwa na muzimu wa muziki wa Ngoma Africa Band ambayo kila pembe imekuwa tishio la kimataifa pamoja na kuachia nyimbo nyingi katika santuri au CDs zao single CD mpya "Awamu ya Tano Uwanjani" ambayo pia imeletwa katika vituo vya redio hapa nchini Tanzania ndio wanayaotamba nayo. 

Bendi hiyo iliyobatizwa majina mengi ya kiusanii na washabiki wake likiwemo jina la "Watoto wa Mbwa" (hawabebeki katika pakacha) imekuwa ni tahasisi inayomilikiwa na washabiki na kuongozwa na Kamanda Ras Makunja ambaye aliwahi kukaliliwa akisema kama angejua ukubwa wa alichokianzisha angechomoa mapema lakini wapi achomoki tena kwa shinikizo la washabiki.

 Muziki wa dansi toka uswahilini unakubalika kimataifa bila kigugumizi, FFU-ughaibu Ngoma Africa band ungana nao at www.ngoma-africa.com au www.facebook.com/ngomaafricaband

No comments:

Post a Comment

Pages