Dar es Salaam, Tanzania, Kampuni inayoongoza kwa maisha ya kidigitali Tigo Tanzania,
leo imeongeza wigo wa upatikanaji wa huduma za mtandao wenye kasi ya juu zaidi nchini
baada ya kuzindua teknolojia ya 4G+.
Uzinduzi wa mtandao wa 4G+ unathibitisha kuwa Tigo ni
kampuni pekee ya mawasiliano inayofanya ubunifu unaoboresha huduma zake kuendana
na mahitaji halisi ya wateja nchini kote.
‘Uzinduzi wa 4G+ ni sehemu ya safari ya mabadiliko ya kidigitali
yanayoongozwa na Tigo hapa nchini. Lengo letu ni kuwawezesha wateja kufurahia
huduma bora zaidi za kidigitali. Daima tuko mbele katika kuleta teknologia za
kisasa za mawasiliano nchini,’ Afisa Mkuu wa Tigo – Teknologia na Mawasiliano Jerome
Albou aliwaambia waandishi wa habari katika uzinduzi wa mtandao wa Tigo 4G+ jijini
Dar es Salaam.
Sasa wateja wa Tigo wanaweza kufurahia huduma bora,
za uhakika na zenye kasi ya juu zaidi ya kupakua maudhui kutoka kwenye mtandao
kwa gharama zile zile. Ili kufurahia mtandao wa 4G+, mteja anahitaji kuwa na simu
yenye uwezo wa 4G+.
Teknologia
ya kisasa ya Tigo 4G+ inaongeza wigo wa matumizi ya huduma za kidigitali nchini.
Teknologia hii inapanua utoaji wa huduma za intaneti yenye kasi ya juu zaidi,
pamoja na kutoa huduma za sauti zinazoendana na mabadiliko ya maisha.
‘Kampuni yetu inajivunia kuzindua teknolojia ya 4G+ inayoiweka
Tanzania katika ramani ya teknolojia ya mawasiliano duniani. Sasa tunashindana
na nchi zilizoendelea ambazo tayari zinawekeza katika teknolojia ya 5G.
Kupatikana kwa teknolojia ya kisasa ya mawasiliano nchini Tanzania kunaibua
fursa mpya za matumizi ya mtandao kwa wateja wetu,’ Afisa Mkuu wa Biashara - Tigo, Tarik Boudiaf alibainisha.
Mbali na kujivunia mtandao wa 4G ulionea katika miji
22 nchini, mtandao wa Tigo 4G+ tayari unapatikana katika miji ya; Dar es
Salaam, Arusha, Kilimanjaro, Moshi na Dodoma, hata hivyo mipango ya kuendelea kuupanua
mtandao huo kufikia miji mingine zaidi nchini inaendeliea. Wateja wanaotumia simu zenye uwezo wa 4G+ sasa
wanaweza kufurahia kasi ya juu zaidi ya kupakua maudhui mbali mbali kwa gharama
zile zile za intaneti.
Mtandao wenye kasi ya juu zaidi wa Tigo 4G+ una kasi mara mbili ya ule
wa Tigo 4G, kwani Tigo 4G ina kasi ya
60Mbps ilihali mtandao mpya wa Tigo 4G+ unaweza kufikia kasi ya hadi 120Mbps.
Kwa ujumla, wateja wanaotumia Tigo 4G+ katika eneo husika hugawana kasi hii ya
juu zaidi miongoni mwao.
Katika
juhudi za kuboresha na kupanua huduma za kidigitali nchini, Tigo ilikuwa mojawapo
ya kampuni za mawasiliano za kwanza kabisa kuwekeza katika teknolojia ya 3G na 4G ambapo Tigo ndio kampuni pekee yenye
mtandao mpana zaidi wa 4G nchini.
Tigo pia ilikuwa ya kwanza kuzindua simu
janja yenye lugha ya Kiswahili pamoja na huduma ya Facebook kwa lugha ya
Kiswahili iliyoongeza matumizi ya huduma za kidigitali kwa idadi kubwa ya
Watanzania wanaotumia lugha ya Kiswahili kwa mawasiliano yao ya kila siku.
No comments:
Post a Comment