HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

September 12, 2018

RAIS DKT. MAGUFULI AMUAPISHA MKURUGENZI MKUU WA TAKUKURU, KATIBU MKUU WA WIZARA YA AFYA PAMOJA NA BALOZI MMOJA IKULU YA CHAMWINO JIJINI DODOMA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Kamishna Diwani Athuman Msuya kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa TAKUKURU katika Ikulu ya Chamwino jijini Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Dkt. John Kiang’u Jingu kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto katika hafla fupi iliyofanyika katika Ikulu ya Chamwino jijini Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Dkt. Azizi Mlima kuwa Balozi wa Tanzania nchini Uganda katika hafla fupi iliyofanyika katika Ikulu ya Chamwino jijini Dodoma.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. John Kiang’u Jingu wa kwanza kulia, akifatiwa na Balozi wa Tanzania nchini Uganda Dkt. Azizi Ponary Mlima pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa TAKUKURU Diwani Athuman Msuya wakila Kiapo cha Uadilifu mara baada ya kuapishwa katika Ikulu ya Chamwino jijini Dodoma.
Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa TAKUKURU Diwani Athuman Msuya akizungumza mara baada ya kuapishwa katika Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na viongozi mbalimbali mara baada ya tukio la Uapisho lililofanyika katika Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa TAKUKURU Diwani Athuman Msuya pamoja na Balozi mteule Valentino Mlowola mara baada ya tukio la Uapisho katika Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. John Kiang’u Jingu wa kwanza kulia, akifatiwa na Balozi wa Tanzania nchini Uganda Dkt. Azizi Ponary Mlima pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa TAKUKURU Diwani Athuman Msuya waki tia saini kwenye hati ya Uadilifu katika Ikulu ya Chamwino jijini Dodoma.
PICHA NA IKULU.

No comments:

Post a Comment

Pages