Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiagana na wananchi wa kijiji cha
Mpwayungu wilayani Chamwino baada ya kuhutubia mkutano wa hadhara
kijijini hapo, Oktoba 20, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa
amemuagiza Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Bilinith Mahengeampeleke Afisa
Kilimo wa mkoa Bw. Bernad Abraham akakague mradi wa umwagiliaji wa
Mpwayungu wilayani Chamwino ili kubaini waliohusika na ubadhilifu wa sh.
bilioni 1.2 za mradi huo.
Alitoa
agizo hilo jana jioni (Jumamosi, Oktoba 20, 2018) baada ya mbunge wa
jimbo Mtera, Livingstone Lusinde kumuomba awasaidie kuhusu upotevu wa
sh. bilioni 1.2 zilizotolewa kwa ajili ya mradi wa umwagiliaji ambazo
matumizi yake hayajulikani.
Waziri
Mkuu ambaye alikuwa katika ziara ya kikazi wilayani Chamwino, Dodoma
alipokea ombi hilo la mbunge wakati akizungumza na wananchi wa Tarafa ya
Mpwayungu, kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji cha
Mpwayungu.
Alisema
mara baada ya Afisa Kilimo, Bw. Abraham kukamilisha ukaguzi wa mradi
huo wa umwagiliaji apelekewe taarifa ili waliohusika na ubadhilifu wa
kiasi hicho cha fedha wachukuliwe hatua kwa mujibu wa sheria.
Katika hatua nyingine,
Waziri Mkuu alivunja kamati ya kusimamia huduma maji ya kijiji cha
Mpwayungu na alimuagiza Mhandisi wa Maji wa wilaya ya Chamwino Bw.
Godfrey Mbabaye aunde kamati mpya.
Waziri
Mkuu alichua hatua hiyo baada ya kutoridhishwa na utendaji wa kamati
hiyo ambayo ilishindwa kutekeleza majukumu yake ikiwemo ujenzi wa vituo
vya kuchotea maji licha ya kukusanya sh. milioni 20 kwa mwezi, mradi huo
unavituo vinne tu.
Alisema
kitendo cha kamati hiyo kushindwa kuongeza kujenga vituo vingine vya
kuchotea maji licha ya kukusanya fedha nyingi kwa mwezi kinasababisha
malalamiko kutoka kwa wananchi ambao ndio wanufaika wa mradi huo.
Pia
Waziri Mkuu alimuagiza mhandisi huyo aombe taarifa ya akaunti ya benki
ya mradi huo ili kubaini katika mfuko wa mradi huo una fedha kiasi na
ndipo aunde kamati mpya ya maji ambayo anatakiwa ashirikishe wanawake
kwa kuwa wao ndio wahusika wakuu.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
S. L. P. 980,
41193 – Dodoma
JUMAPILI, OKTOBA 21, 2018.




No comments:
Post a Comment