Chama cha Skauti Tanzania kimeandaa kambi ya Kitaifa ya Jamboree ya Hewani itakayofanyika mkoani Tanzania kuanzia tarehe 19 hadi 21 Oktoba 2019.
Jamboree ya Hewani ya Kimataifa ni kambi ambayo skauti duniani kote huwasiliana na skauti wenzao kwa kutumia Mawasiliano ya Radio pamoja na Mtandao wa intanet maarufu kama JOTA JOTI.
Hii ni mara ya kwanza kwa Skauti mkoa wa Tanga kuwa wenyeji wa Jamboree hii, kwani mara nyingi imekuwa ikifanyika kitaifa katika mikoa mingine kama vile D’salaam, Arusha, Morogoro, Dodoma, Simiyu, na Zanzibar.
Akizungumza na vyombo vya habari ofisini kwake, Kamishna wa Skauti Mkoa wa Tanga Bi. Upendo Mbwambo amesema amefurahishwa sana na uamuzi wa Makao Makuu ya Chama cha Skauti Tanzania kupanga kambi hii ifanyike kitaifa mkoani Tanga.
“Uongozi wa Skauti mkoani Tanga tumefurahishwa sana na uamuzi wa Makao Makuu ya Skauti kuamua Jamboree ya Hewani ya Kimataifa ifanyike mkoani Tanga” alisema b. Mbwambo.
Mkoa wa Tanga umekuwa na bahati ya kuwa wenyeji wa matukio ya kitaifa kama vile, Wiki ya Vijana Kitaifa, Kumbikizi ya Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius K. Nyerere, pamoja na shughuli za kilele cha mbio za Mwenge wa Uhuru ambazo zote hizo zilifanyika kitaifa mkoani Tanga wiki iliyopita.
Jamboree ya Hewani ya Skauti kitaifa itafanyika katika eneo la shule ya Sekondari ya Masechu iliyopo Kisosora katika Manispaa ya Tanga.
Skauti kutoka wilaya zote za mkoa wa Tanga pamoja na mikoa jirani watahudhuria kambi hii ambayo Mgeni Rasmi katika ufunguzi wa kambi hii anatarajiwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Mhe. Martin Shigela ambaye kwa mujibu wa Katiba ya Chama cha Skauti Tanzania yeye ni Mlezi wa Skauti katika ngazi ya Mkoa.
Tayari Viongozi Waandamizi wa Skauti kutoka Makao Makuu ya Skauti Tanzania wapo mkoani Tanga tangu juzi kufuatilia na kuhakikisha maandalizi ya kambi hiyo yanakwenda vizuri, jumla ya skauti 3000 wanatarajia kushiriki kambi hii, alisema Bi. Upendo Mbwambo Kamishna wa Skauti wa Mkoa wa Tanga.

No comments:
Post a Comment