HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

January 30, 2019

FIRST SERIES OPEN TRIAL CROSS COUNTRY-ARUSHA

NA MWANDISHI WETU

SERIES ya kwanza kuelekea Mashindano ya Wazi ya Cross Country Taifa inatarajiwa kufanyika viwanja vya Magereza Kisongo jijini Arusha Jumamosi Februari 2 mwaka huu.

Kwa mujibu wa Katibu wa Chama cha Riadha Mkoa wa Arusha (ARAA), Alfredo Shahanga, maandalizi kuelekea mashindano hayo yanakwenda vema.

Shahanga, alisema klabu mbalimbali tayari zimetaarifiwa kuhusu mashindano hayo na wanariadha wako kwenye utayari wa kushindana.

“Huu ni mwanzo wa ‘series’ za Cross Country ikiwa ni maandalizi ya kuelekea mashindano ya Dunia, hivyo tutaanza Jumamosi na ni mashindano ya wazi hivyo mtu yeyote anaruhusiwa kushiriki na hakuna kiingilio,” alisema Shahanga.

Katibu huyo, alisema baada ya Jumamosi yatafuata Mashindano ya Wazi ya Taifa mjini Moshi, Kilimanjaro Februari 16 kwenye viwanja vya Gofu.

Alitaja mbio zitakazoshindaniwa kuwa ni Kilomita 10 kwa wanaume na wanawake Sr, wanaume Jr watashindana Kilomita 8 na wanawake Jr itakuwa ni Kilomita 6.

Shahanga, alisema kwa mujibu wa uongozi wa Shirikisho la Riadha Tanzania (RT), ‘series’ zote zimepata ufadhili wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA).

Alisema kutakuwa na zawadi kwa washindi sita wa kwanza katika kila ‘categories’ katika mbio hizo.

Mashindano ya Cross Country ya Dunia yanatarajiwa kufanyika huko Aarhus nchini Denamark, Machi 30 mwaka huu.

No comments:

Post a Comment

Pages