Mkurugenzi wa Chuo cha Madaktari Wasaidizi Ifakara mkoani Morogoro Prof. Frola Kessy akielezea
changamoto ya wahudumu wa afya katika kutoa takwimu sahihi na namna ya
kuepuka na changamoto hiyo katika mkutano wa wadau wa afya mkoani
Morogoro.
Wadau
wa afya na wakufunzi kutoka vyuo mbalimbali hapa nchini ikiwemo chuo
kikuu cha Mzumbe ,chuo kikuu cha Dodoma ,kituo cha kimataifa cha mafunzo
ya afya Ifakara na chuo kikuu cha Mhimbili wakifatilia kwa umakini
mjadala wa namna takwimu zinazokusanywa jinsi ambavyo zinavyoshindwa
kutumiwa ipasavyo na wahudumu wa afya.
Mtakwimu
mkuu ofisi ya Rais tawala za mikoa na serikali za mitaa(TAMISEM)
Yasinta Kijuu akiwasilisha kwa wadau wa afya namna ambavyo serikali
iliona mifumo ya takwimu usivyotumiwa ipasavyo na kuangalia jinsi ya
kutatua changamoto hiyo katika mkutano wa wadau wa afya uliofanyika
mkoani Morogoro ambapo alisema mwaka 2016 ndipo mchakato wa kutatua
changamoto hiyo ya matumizi ya takwimu ulianza.
Wadau
wa afya wakimfatilia kwa umakini katika mkutano wa wadau wa afya mkoani
Morogoro mkufunzi wa chuo kikuu Mzumbe Dr,Mackfallen Anasel
akizungumzuia jinsi ambavyo mitaala ya kufundishia inahitaji marekebisho
katika swala la ukusanyaji na matumizi ya takwimu ili wahitimu wa
vyuo waelewe matumizi sahihi ya takwimu hizo .
Makamu
mkuu wa chuo taaluma,utafiti na ushauri kutoka chuo cha serikali za
mitaa Hombolo Dodoma Dr, Michael Msendekwa akitoa ushauri wa jinsi
gani ya kufikia utoaji wa huduma sahihi za afya kwa wananchi na jinsi ya
kuodoa vikwazo vinavyo kwamisha matumizi sahihi ya takwimu katika
kutoa maamuzi katika kikao cha wadau wa afya mkoani Morogoro.
No comments:
Post a Comment