HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

January 26, 2019

JAJI MKUU: KESI ZENYE DOSARI ZISIINGIE KATIKA MFUMO WA MAHAKAMA

NA JANETH JOVIN

JAJI Mkuu wa Tanzania Profesa Ibrahimu Juma amewataka wasajili wa mahakama zote nchini kuhakiksha  kesi zenye dosari haziingii kwenye mfumo wa mahakama yoyote hapa nchini.

Profess Juma,  ameyasema hayo jijini  Dar e Salaam Januari 26, 2019 wakati akizungumza na waandishi wa habari juu ya maadhimisho ya wiki na siku ya sheria nchini, ambayo hufanyika kila mwanzoni mwa mwaka yanayoashiria kuanza rasmi kwa mwaka wa Mahakama. 

Alisema kumekuwa na malalamiko kutoka kwa wananchi kuhusu Mahakama ya Rufaa pamoja na Mahakama Kuu kutupilia mbali mashauri mbalimbali yanayopelekwa ambapo amebainisha kuwa hali hiyo inatokana na dosari zinazojitokeza katika kesi hizo.

"Muhimili wa mahakama upo wazi sana, kila.kitu tunachokifanya kinapimika, unapofungua kesi unapewa muda wa kujibu, unaleta mashahidi, kesi inarekodiwa, hukumu inatolewa,

"Hatupendezwi na malalamiko ya jumla jumla kwani kuna mfumo wa kupokea malalamiko, sisi tupo wazi na 
Huwezi kuwazuia Wanasiasa wasizungumze ndio kazi yao, sisi tunafanya kazi kimya kimya na ukitaka majibu utayakuta katika nyaraka" alisema Jaji Profesa Juma

Aidha Jaji Juma amemsifu  Msajili aliyesimama kidete kukataa kusajili kesi yenye dosari, "nampongeza kwa ujasiri, tuna Majaji wachache hatutaki kuwapangia kesi nyingi kisha wazifute" alosema Jaji Mkuu. 

Aidha Jaji Profesa Juma alisema  mashauri mengi ya kesi yanachelewa kumalizika kutokana na uelewa mdogo wa wannchii ikiwa ni pamoja na kutokufahamu miongozo ya mashauri mbalimbali paomja na haki zao

Kwa upande mwingine, Jaji profesa Juma amewataka  wananchi ambao wamezoea kubeba mabango ya malalamiko siku ya kilele cha wiki ya sheria waache kufanya hivyo na badala yake watumie wiki ya sheria kutafuta suluhu ya malalamiko hayo.

Wiki ya Sheria kwa  mwaka huu Kitaifa itafanyikia jijini Dodoma katika viwanja vya Nyerere Square kuanzia Januari 31 na kuitimishwa Februari 6, 2019 jijini Dar es Salaam. 

Rais wa Jamuhuri ya Nyumbani wa Tanzania Dk.  John Pombe Magufuli anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika siku ya kilele hicho ambacho kauli mbiu yake itakuwa ni, *Utoaji wa Haki kwa wakati: wajibu wa Mahakama na wadau*.

No comments:

Post a Comment

Pages