Jengo
la nyumba za walimu katika shule ya Kizimkazi Kusini Unguja
lililojengwa kwa nguvu za wananchi na ufadhili wa MultiChoice Tanzania
iliyochangia takriban shilingi milioni 120 katika ujenzi huo.
Waziri
wa Habari Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar Mahmoud Thabit Kombo (wa
pili Kulia. Mku wa Mkoa wa Kusini Unguja Hassan Khatib
Hassan. (Kulia), Naibu Katibu Mkuu wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali
Madinnah na Mkurugenzi Mtendaji wa MultiChoice Tanzania Jacqueline
Woiso (Kushoto) wakiwasili katika shule ya Kizimkazi tayari kufungua
rasmi jengo la nyumba za walimu katika shule
ya Kizimkazi Kusini Unguja jana. Jengo hilo lenye nyumba mbili za
walimu limejengwa kwa nguvu za wananchi na ufadhili wa MultiChoice
Tanzania iliyochangia takriban shilingi milioni 120 katika ujenzi huo.
Waziri
wa Habari Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar Mahmoud Thabit Kombo (Kulia)
na Mkurugenzi Mtendaji wa MultiChoice Tanzania Jacqueline Woiso
(Kushoto) wakikata utepe kufungua rasmi jengo la nyumba za walimu katika
shule ya Kizimkazi Kusini Unguja jana. Jengo hilo
lenye nyumba mbili za walimu limejengwa kwa nguvu za wananchi na
ufadhili wa MultiChoice Tanzania iliyochangia takriban shilingi milioni
120 katika ujenzi huo.
Waziri
wa Habari Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar Mahmoud Thabit Kombo (wa
tatu kulia - waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi
Mtendaji wa MultiChoice Tanzania Jacqueline Woiso (wa pili kulia) na
maafisa mbalimbali waandamizi wa Zanzibar muda mfupi
baada ya kufungua rasmi jengo la nyumba za walimu katika shule ya
Kizimkazi Kusini Unguja jana. Jengo hilo lenye nyumba mbili za walimu
limejengwa kwa nguvu za wananchi na ufadhili wa MultiChoice Tanzania
iliyochangia takriban shilingi milioni 120 katika
ujenzi huo.
Waziri
wa Habari Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar Mahmoud Thabit Kombo
akipokea seti ya DStv kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa MultiChoice
Tanzania Jacqueline Woiso kwa ajili ya kufungwa kwenye nyumba mpya za
walimu wa shule ya Kizimkazi Kusini Unguja. MultiChoice Tanzania
imefadhili ukamilishaji wa jengo lenye nyumba mbili za walimu ambapo
imechangia takriban shilingi milioni 120 katika ujenzi
huo.
Na Mwandishi Wetu, Zanzibar
Na Mwandishi Wetu, Zanzibar
Kampuni ya MultiChoice Tanzania,
imekabidhi jengo la nyumba mbili za walimu katika shule ya Kizimkazi
Kusini Unguja Zanzibar katika hafla iliyofanyika shuleni hapo hivi
karibuni na kuongozwa na Waziri wa Habari, Utalii na Mambo ya Kale
Mahmoud Thabit Kombo na Mkurugenzi Mtendaji wa MultiChoice
Tanzania Jacqueline Woiso.
Ujenzi wa nyumba hizo za kisasa za walimu ulifanywa na wananchi wa Kizimkazi na kufadhiliwa na MultiChoice Tanzania
ambayo ilichangia takriban shilingi milioni 120 katika kukamilisha mradi huo.
Akizungumza
wakati wa ufunguzi rasmi wa nyumba hizo, Waziri Kombo ameelezwa
kurudhishwa kwake na kiwango cha ujenzi
wa nyumba hizo na kubainisha kuwa mradi huo umekamilika kwa haraka na
kwa kiwango cha hali ya juu kutokana na mchango mkubwa wa MultiChoice
Tanzania.
Kwa
upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa MultiChoice Tanzania Jacqueline
Woiso amesema mradi huo ni muendelezo wa uwekezaji
mkubwa wa MultiChoice katika miradi ya kijamaa kote nchini.
“MultiChoice imekuwa ikiwekeza fedha nyingi katika sekta mbalimbali za
kijamii ikiwamo elimu, na ufadhili huu ni ishara tosha ya ushiriki wetu
katika kuleta maendeleo ya jamii yetu”.
Pia
Mkurugenzi huyo aliridhia ombi la Waziri Komba kuiomba MultiChoice
Kuchangia katika kuseka samani katika nyumba hizo. Pia MultiChoice
ilitoa seti za ving’amuzi vya DStv kwa ajili ya kufungwa katika nyumba
hizo ili kuwawezesha walimu kupata habari burudani na elimu mbalimbali
kupitia DStv na hivyo kupanua zaidi ufahamu wao na hatimaye kuwa walimu
bora zaidi.
hule
ya Kizimkazi ina wanafunzi takriban 800 na ina madarasa ya awali,
msingi na Sekondari na miongomi mwa shule kongwe kabisa katika
kisiwa cha Unguja.
No comments:
Post a Comment