Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali
Mohamed Shein, akiwapungua Mkono Wananchi akiwa katika gari Maalum ya
Jeshi la Wananchi Tanzania JWTZ, wakati akiingia katika Uwanja wa
Gombani Kisiwani Pemba kuhudhuria Maadhimisho ya Miaka 55 ya Mapinduzi
ya Zanzibar, akiwa Mkuu wa Brigedi ya Nyuki Zanzibar, Brigedia Jenerali
Fadhil Omar Nondo. (Picha zote na Ikulu)
Askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania JWTZ, wakionesha jinsi ya
uchezaji wa Gwarige la kimya, wakati wa Sherehe za Miaka 55 ya Mapinduzi
ya Zanzibar zilizofanyika Uwanja wa Gombani.
Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein,
akiwahutubia wananchi wakati wa sherehe za miaka 55 ya Mapinduzi ya
Zanzibar, zilizofanyika katika Uwanja wa Gombani Kisiwani Pemba.
Mke
wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar marehemu Abeid Amani Karume,
Mama Fatma Karume, Mke wa Rais Mstaafu wa Tanzania, Mama Anna Mkapa na
Mke wa Rais Mstaafu wa Zanzibar, Mama Shadya Karume, wakifuatilia hotuba
ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali
Mohamed Shein, katika Uwanja wa Gombani Kisiwani Pemba.
Askari
wa Jeshi la Polisi Zanzibar, wakionesha jinsi ya uchezaji wa gwaride la
zamani, wakati wa sherehe za Miaka 55 ya Mapinduzi ya Zanzibar,
zilizofanyika katika Uwanja wa Gombani.
Askari
wa Kikosi cha KMKM wakitoa heshima wakiwa katika mwendo wa kasi wakati
wa maadhimisho ya Miaka 55 ya Mapinduzi ya Zanzibar, katika Uwanja wa
Gombani Pemba.
Kikosi cha Makomandoo wa JWTZ wakipita kwa ukakamavu wakati wa
Maadhimisho ya Sherehe za Miaka 55 ya Mapinduzi ya Zanzibar, Uwanja wa
Gombani Pemba.
No comments:
Post a Comment