Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotions, Alex Msama, akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo kuhusu Tamasha la Pasaka litakaloanza kutimua vumbi Aprili 21 jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mratibu wa tamasha hilo, Jimmy Charles. (Picha na Francis Dande).
Mkurugenzi
wa Kampuni ya Msama Promotions, Alex Msama, akizungumza na waandishi wa
habari jijini Dar es Salaam leo kuhusu Tamasha la Pasaka litakaloanza
kutimua vumbi Aprili 21 jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mratibu wa
tamasha hilo, Jimmy Charles.
NA MWANDISHI WETU
KAMATI ya Maandalizi ya Tamasha la Pasaka chini ya Mwenyekiti wake Alex Msama, imeanza kuzunguma na waimbaji wa kimataifa kwa ajili ya kushiriki tukio hilo la kenye hadhi ya kimataifa litakaloanza kutimua vumbi Aprili 21, mwaka huu jiji Dar es Salaam.
Mbali ya Tamasha hilo linalofanyika kila mwaka chini ya kampuni ya Msama Promotions ya jijini Dar es Salaam, kubeba maudhui ya kueneza ujumbe wa injili ya Mungu kwa mataifa yote kupitia sauti za vinanda na vinubi, pia limekuwa faraja kwa makundi maalumu katika jamii.
Faraja ni kutokana na Kamati hiyo kuwa na utaratibu wa kutoa sehemu ya mapato ya viingilio vya ukumbini kufariji wenye mahitaji maalumu kama yatima, walemavu na wajane iwe kabla ama baada ya tukio lenyewe.
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Msama alisema Kamati yake imeshaanza kazi na tayari imeanza kuzungumza na waimbaji wa kimataifa na yanakwenda vizuri, ingawa alisema si wakati wa kuwataja waimbaji wenyewe wala nchi wanazotoka.
“Maandalizi ya Tamasha yanakwenda vizuri. Tayari tumeanza kufanya mazungumzo na waimbaji wa nje. Nashukuru mazungumzo yanakwenda vizuri, majina na nchi wanazotoka, tutawaeleza kwa siku zijazo,” alisema.
Kati ya waimbaji wa kimataifa waliowahi kushiriki tamasha hilo, ni Sipho Makhabane, Solly Mahlangu, Rabecca Malope (Afrika Kusini); Ephraem Sekereti (Zambia), Kwetu pazuri (Rwanda), Solomon Mukubwa na Anastazia Mukabwa wa Kenya pamoja na Faraja Ntaboba (DR Congo).
Aidha, Msama ametoa wito kwa wadau wa muziki wa injili kukakaa mkao wa kupokea baraka za Mungu kupitia tamasha hilo litakalopambwa na waimbaji wa ndani na nje ya nchi ili kuisindikia Pasaka.
Alisema Tamsha la mwaka huu, litakuwa la tofauti kwa sababu wamejipanga vizuri kuhakikisha linakuwa la kimataifa zaidi kuanzia maandalizi yake, aina ya waimbaji na kwamba kila mwimbaji atakayeopanda jukwaani ataimba live.
Msama alisema kwamba, baada ya Tamasha hilo kuzinduliwa katika jiji la Dar es Salaam Aprili 21, kishindo hicho kitahamia mikoani kwa kunzia jiji la Dodoma ambalo limeteuliwa kuwa la kwanza kabla ya tujui hilo kushambulia mkoa mmoja baada ya wingine.
Alisema kwa miaka miwili, tamasha hilo lilihama katika jiji la Dar Salaam kutokana na sababu ambazo zilikuwa nje ya uwezo wao, hivyo ni muhimu kwa wadau wa jiji hilo kujitokeza kwa wingi katika tamasha la safari hii litakalobeba vionjo vingi.
Alisema mbali ya kueneza ujumbe wa Neno la Mungu, pia Tamasha la mwaka huu, linafanyika chini ya kaulimbiu ya “Umoja na Upendo hudumisha amani na nchi yetu,” kutokana na ukweli kuwa jambo la maendeleo linaloweza kufanyika kama hakuma amani na umoja.
No comments:
Post a Comment