Baadhi ya wakazi wa Moshi na maeneo jirani
wakiwa wamejikokeza katika hoteli ya Keys kuchukua namba zao za ushiriki wa mbio
za Kilimanjaro Premium Lager Marathon 2019.
KILIMANJARO, TANZANIA
Mamia ya
wakazi wa Moshi na maeneo ya jirani wamejitokeza katika Hoteli ya Keys kuchukua
namba za ushiriki wa mbio za Kilimanjaro Premium Lager Marathon 2019
zinazotarajiwa kufanyika Jumapili hii katika Chuo Kikkuu Cha Ushirika Moshi (MoCU).
Kwa mujibu
wa waandaaji wa mbio hizo maarufu,
muitikio ni mkubwa sana kama ilivyokuwa Dar es Salaam na Arusha huku zikiwa
zimebaki takriban siku tatu kabla ya tukio hilo ya aina yake huzu zoezi hilo la
ugawaji likitarajiwa kumalizaika leo.
“Tutatoa nafasi pia Machi 1 (saa nne hadi saa kumi na moja
na Machi 2 (saa tatu asubuhi hadi saa sita mchana) kwa ambao hawatakua
wamechukua namba zao za ushiriki kufanya hivyo pale Keys hotel na tunasisitiza
kuwa hatkutakuwa na usajili siku ya mashindano,” walsema waandaaji hao.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, maandalizi yote yamekamilika
sasa na mbio hizo zinatarajiwa kushirikisha wakiambiaji zaidi ya 10,000 kutoka
nchi 50 tofauti.
Tayari kuna pilka pilka mbali mbali katika Mji wa Moshi huku
hoteli nyingi na sehemu za kulala wageni zikiwa zimejaa hadi wiki ijayo.
Mkuu wa Wilaya ya Moshi, Kippi Warioba walisifia mbio za
Kilimanjaro Marathon na kusema ndio
tukio kubwa zaidi Mjini hapo na kama wilaya wamejianfdaa vizuri kuhakikisha
kuna ulinzi wa kutosha kwa sababu kutakuwa na wageni wengi wiki hii.
“Hili ni tukio kubwa na linahitaji mpangilio mzuri ili
kuhakikisha washiriki na mali zao wako salama,” alisema Mkuu huyo wa Wilaya
punde baada ya kupokea namba yake ya ushiriki wa mbio za kilomita 5.
Mgeni rasmi katika mbio za mwaka huu ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na
Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe.
Wadhamini
wa mwaka huu ni Kilimanjaro Premium Lager, wakiwa wadhamini wa mbio za kilomita
42, Tigo mbio za kilomita 21 na Grand Malt Kilomita 5 Fun na wadhamini wa meza
za maji KK Security, Keys Hotel, Kilimanjaro Water, TPC Sugar, Simba Cement,
AAR, Kibo Palace, Barclays Bank, Precision Air na CMC Automobiles.
No comments:
Post a Comment