Baadhi ya waombolezaji.
Watu mbalimbali wakiwa katika msiba wa Ruge Mutahaba.
Waombolezaji.
Ndugu, jamaa na marafiki wakiwa na huzuni.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda na akiwa na waombolezaji wengine katika msiba wa Ruge Mutahaba.
Baba mzazi wa marehemu Ruge Mutahaba, Prof. Mutahaba (katikati) akiwa na waombolezaji wengine nyumbani kwake Mikocheni jijini Dar es Salaam.
Msanii wa Muziki wa Kizazi Kipya Kala Jelemiah akisalimiana na mbunge wa Singida Magharibi, Mwigulu Nchemba.
Mkurugenzi wa CMG, Joseph Kusaga, akizungumza na waandishi wa habari.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda,akisalimiana na Mkurugenzi wa CMG, Joseph Kusaga.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, akizungumza na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Daniel Chongolo na Mkurugenzi wa CMG, Joseph Kusaga.
Baadhi ya waandishi wa habari wakiwa katika msiba wa marehemu Ruge.
Waziri Mkuu akiwasili nyumbani kwa Prof. Mutahaba.Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akisalimiana na Mkurugenzi wa Clouds Media Group, Joseph Kusaga.
Waziri Mkuu akiwasili nyumbani kwa Prof. Mutahaba.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akisaini kitabu cha maombolezo.
Baadhi ya waombolezaji.
Kiongozi wa ACT Wazalendo akisalimiana na mmoja wa wafanyakazi wa Clouds Media Group.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akiteta jambo na baba mzazi wa marehemu Ruge Mutahaba.
Kiongozi wa ACT Wazalendo akiteta jambo na Ismail Jussa Ladhu.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akitoa salama za serikali katika msiba wa Ruge Mutahaba.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akimpa mkono wa pole baba mzazi wa marehemu Ruge Mutahaba.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiagana na baba mzazi wa marehemu Ruge Mutahaba.
Msafara wa waziri mkuu ukiondoka.
WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa amesema
Taifa limepoteza kijana aliyekuwa msatari wa mbele kuwahamasisha vijana
wajitambue wawe wazalendo kwa nchi yao na watambue fursa za maendeleo zilizopo na
wasiwe walalamikaji.
Ameyasema hayo leo (Jumatano,
Februari 27, alipokwenda kuhani msiba wa aliyekuwa Mkurugenzi wa Vipindi na
Uzalishaji wa Clouds Media Group, Ruge Mutahaba kwa niaba ya Serikali, nyumbani
kwa wazazi wa marehemu Mikocheni jijini Dar es Salaam.
Waziri Mkuu amesema vijana nchini walikuwa na
kiongozi aliyekuwa akiwaongoza kwa kuwafungua kimawazo na kuwaonesha fursa
mbalimbali zitakazowawezesha kuwakwamua kifikra na kiuchumi ili waweze
kujitegemea.
Waziri Mkuu amesema msiba huo
ni wa wote kwani marehemu amefanya kazi kubwa ya kushirikiana na Serikali
kuhamasisha vijana kujitambua na kutambua fursa zilizpo na kuzifanyia kazi.
“Ruge ametoa mchango mkubwa kwa Taifa
Amesema marehemu Ruge katika kipindi cha uhai
wake amefanya kazi kubwa kwa upande wa Serikali, kuanzia awamu ya nne hadi ya
tano hususani katika suala la kuhamasisha vijana kujikwamua na kutokuwa
wategemezi.
Pia, Waziri Mkuu amesema
historia yake inaeleza namna alivyozunguka nchi nzima na kukutana na makundi ya
vijana mbalimbali na kuwaelimisha namna ya kutambua fursa zilizopo nchini huku
akiwahamasisha wawe wazalendo.
"Marehemu alikuwa akitoa hadi fedha zake
binafsi kwa ajili ya kuwawezesha vijana hasa wale ambao hawakuwa na uwezo wa
kiuchumi ili nao washiriki katika shughuli mbalimbali za ujasiriamali na
hatimaye waondokane na utegemezi.”
Kadhalika, Waziri Mkuu ametoa wito kwa wazazi,
watoto wa marehemu pamoja na wananchi kwa ujumla waendelee kuwa na subira na
watulivu katika kipindi hiki kigumu cha kuondokewa na mpendwa wao.
No comments:
Post a Comment