MATESO Modesti (35^)
wa Zanzibar ameibuka mshindi wa Bonasi ya Jackpoti kutoka SportPesa mara baada
ya kushinda kwa usahihi ubashiri wake wa mechi 11 kati ya 13 ambazo amebashiri
na kushinda shilingi 6,835,003
Modesti ni
mfanyabiashara wa matunda huko Visiwani Zanzibar maeneo ya Darajani ambaye mara
nyingi amekuwa akicheza michezo ya ubashiri SportPesa bila ya mafanikio ya
kushinda kabla ya juzi kushinda.
Akizungumza na Waandishi
wa Habari, Modesti alisema kuwa “Nilianza kucheza SportPesa, mwaka jana na
ninashukuru kufanikiwa kushinda mwaka huu, kiukweli ilikuwa ndoto yangu
kushinda siku moja bonsai hii, hivyo ninajisikia furaha.
“Baada ya ushindi huu
wa bonasi, nimepanga kuiboresha biashara yangu ya matunda, mimi mfanyabiashara
wa matunda baada ya kufanikiwa kushinda
ubashiri wangu kupitia Kampuni ya SportPesa inayoendeleshwa michezo hiyo ya
ubashiri.
“Nilishinda ubashiri
huu baada ya kushinda mechi 11 kati ya 13 ambazo zimewekwa na SportPesa,, hivyo
nimepanga kuendelea kubashiri zaidi kupitia SportPesa hasa kwenye bonasi hii.
“Na nitacheza zaidi
Jackopti bonasi kutokana na kiwango kikubwa cha fedha kilichowekwa ambacho ni
kingi na uzuri wake ukishinda mechi zako, basi haraka unatumiwa ujumbe kuwa
umeshinda bonasi na fedha unapatiwa.
“Hivyo siyo kampuni ya
kijanjakijanja kama zilivyokuwa kampuni nyingine za kubet, hivyo nawashauri
vijana wenzangu na wazee kucheza kupitia SportPesa,”alisema Modesti aliyepanga
kuboresha biashara ya matunda kupitia biashara hiyo.
Meneja Uhusiano wa
SportPesa Bi. Sabrina Msuya alimpongeza mshindi wa bonasi kwa ushindi wake na
kumshauri pesa alizoshinda awekeze ili aweze kukuza biashara yake ya matunda na
kujiongezea mtaji.
“Wiki hii JackPoti yetu
imesimamia zaidi ya milioni 494,275,700/- ambapo inakaribia kufika nusu bilioni
na tunatarajia kupata mshindi. Mteja anapaswa kuweka ubashiri wake kwa usahihi
wa mechi 13 ili kujishindia kiasi hicho mbali na hapo bonasi hutolewa kwa
watakaopatia mechi kuanzia 10-12.
No comments:
Post a Comment