SHIRIKISHO la Riadha Tanzania (RT), linapenda kuungana na Uongozi na
Wafanyakazi wa Kampuni ya Clouds Media Group (CMG), Familia ya
Wana Tasnia ya Habari na Wadau wote wa michezo, Sanaa na burudani,
kutoa salamu za pole kutokana na msiba mzito wa Mkurugenzi wa
Vipindi na Uzalishaji wa CMG Ndugu Ruge Mutahaba aliyefariki Dunia Februari 26 huko nchini Afrika Kusini alikokuwa akiendelea na
matibabu.
Shirikisho la Riadha la Tanzania, likiwa ni sehemu ya jamii kwa nyakati
tofauti limekuwa likishirikiana vema na kwa ukaribu na CMG katika
utekelezaji wake wa majukumu ya kusimamia na kuendesha mchezo wa
riadha hapa nchini.
RT imekuwa na ushirikiano wa karibu na CMG katika utekelezaji wake wa
majukumu ya kila siku, hivyo taarifa za kifo cha Ruge hakika zimetustua
sisi kama viongozi na familia nzima ya mchezo wa Riadha hapa nchini.
Kutokana na msiba huo mzito tunapenda kutoa salamu za pole kwa
Uongozi, Wafanyakazi wote wa CMG, Wadau wa habari, michezo,
burudani na familia ya Ruge Mutahaba kutokana na kifo cha mpendwa
wetu na kuwaombea kuwa na moyo wa subira katika kipindi hiki kigumu.
Familia ya Riadha nchini, itaendelea kumkumbuka Ruge kutokana na
moyo wake wa kujitolea katika jamii, ubunifu na uhamasishaji wake
katika masuala mbalimbali ya kimaendeleo katika jamii na hakika
tutaendelea kuyaenzi.
1Pia, tutazidi kuendeleza ushirikiano wa karibu tuliokuwa nao na CMG
chini ya Ruge enzi za uhai wake.
Tunarudia tena kutoa salamu za pole kwa wafiwa na kuwaombea katika kipindi hiki kigumu cha kuondokewa na mpendwa wetu. Bwana Alitoa na Bwana Ametwaa, Jina lake lihimidiwe. Amin. Wilhelm Gidabuday Katibu Mkuu RT Februari 27, 2019
No comments:
Post a Comment