NA TIGANYA VINCENT
BENKI ya Posta (TPB) imetoa msaada wa vyandarua
100 na magodoro 25 vyote vikiwa na thamani ya millioni kwa ajili ya Hospitali
ya Wilaya ya Nzega.
Msaada huo umekabidhiwa juzi na
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya Posta Tanzania (TPB) Dkt. Edmund
Mndolwa kwa uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Nzega.
Alisema msaada huo ni sehemu ya kuunga
mkono juhudi za kuboresha afya ya mama na mtoto ndio maana wameamua kutoa kwa
ajili ya wodi ya wanawake na watoto.
Kwa upande wa Mkuu wa Wilaya ya Nzega
Godfrey Ngupula alisema kuwa Benki hiyo imeamua kurudisha sehemu ya mapato yake
katika kuchangia sekta ya afya.
Alitoa wito kwa Taasisi nyingine za
kifedha wilayani humo kusaidia jamii katika ujenzi wa madarasa , ununuzi wa
vifaa tiba na uboresha wa miundo ambayo itasaidia kuwavutia wananchi kujiunga
na huduma zao.
Awali akizindua tawi jipya la TPB
wilayani Nzega, Mkuu wa Mkoa wa Tabora
Aggrey Mwanri amewataka wakazi wa eneo hilo kujenga utamaduni wa
kuhifadhi fedha zao katika Benki ili kuepuka kuvamiwa na kujeruhimiwa na wakati
mwingine kuwawa.
Alisema vitendo vya kukaa na fedha
majumbani vinawaweka katika hatari ya kushambuliwa na majambazi na wakati
mwingine watu wazima kudhalilishwa mbele ya watoto wao.
No comments:
Post a Comment