Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Balozi wa Misri Nchini Ibrahim Abdullah, ofisini
kwake Magogoni Februari 15, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
*Awahakikishia ushirikiano wa kutosha kutoka Serikalini
WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa amewakaribisha wawekezaji kutoka nchi za India,
Misri na Falme za Kiarabu waje wawekeze nchini na Serikali itawapa
ushirikiano wa kutosha.
Ameyasema
hayo leo (Ijumaa, Februari 16, 2019) wakati alipokutana kwa nyakati
tofauti na mabalozi wa India, Misri na Falme za Kiarabu wanaowakilisha
nchi zao hapa Tanzania.
Mabalozi aliokutana nao ni Balozi
Sandeep Arya (India), Balozi Mohamed Abulwafa (Misri) na Balozi
Mohammad Albahri (Kaimu Balozi wa Falme za Kiarabu nchini Tanzania).
Akizungumza
na Mabalozi hao Ofisini kwa Waziri Mkuu, Magogoni, Dar es salam, Waziri
Mkuu amesema Tanzania ipo tayari kuwapokea wawekezaji kutoka kwenye
nchi hizo.
Amesema
Serikali imedhamiria kuendeleza sekta ya viwanda nchini ili kukuza
uchumi na kufikia wa kati ifikapo 2025, hivyo amewakaribisha
wafanyabiashara waje wawekeze.
Amesema
Ofisi yake kupitia Waziri mwenye dhamana ya Uwekezaji, Bibi Angela
Kairuki iko tayari kuwasikiliza na kuwasaidia wawekezaji wote
wanaokusudia kuwekeza nchini.
“Tanzania
iko tayari wakati wote kutoa ushirikiano ili kuhakikisha wawekezaji
watakaojitokeza kuwekeza nchini wanafanikiwa ili mataifa yote yaweze
kufaidika.”
Kadhalika,
Waziri Mkuu amesema Tanzania ina vivutio vingi vya utalii ikiwa ni
pamoja na uwepo wa mlima Kilimanjaro, mbunga zenye wanyama wa aina
mbalimbali na fukwe nzuri.
Hivyo,
ametumia fursa hiyo kuwakaribisha watalii kutoka mataifa mablimbali
yakiwemo yaIndia, Misri na Falme za Kiarabu waje nchini na kutembelea
vivutio vya utalii vilivyopo.
Kwa upande wao,Mabalozi hao wameishukuru
Serikali kwa ushirikiano mzuri uliopo baina ya Tanzania na nchi zao,
hivyo wamemuhakikishia Waziri Mkuu kwamba watauendeleza.
Wamesema
wapo tayari kushirikiana na Tanzania kuhakikisha mkakati wa Serikali wa
kukuza uchumi kutoka wa chini kwenda wa kati kupitia sekta ya viwanda
unafanikiwa.
Pia
Mabalozi hao wameahidi kushirikiana na Serikali Tanzania kuhakikisha
inaboresha sekta mbalimbali ikiwemo ya utalii ili kuongeza idadi ya
watalii wanaotembelea nchini.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
IJUMAAA, FEBRUARI 16, 2019.
No comments:
Post a Comment