HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

February 16, 2019

DKT. MPANGO ATETA NA WAFANYAKAZI NA KUHIMIZA MAADIDLI NA UWAJIBIKAJI KAZINI

Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isidor Mpango (Mb) akizungumza na Watumishi wa Wizara hiyo (hawapo pichani), katika kikao na Watumishi hao Jijini Dodoma.
Baadhi ya Watumishi wa Wizara ya Fedha na Mipango wakifuatilia kwa karibu hoja mbalimbali zilizokuwa zikitolewa katika kikao cha Watumishi wa Wizara hiyo Jijini Dodoma. (Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini WFM).
 
Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Isdor Mpango amekutana na Watumishi wa Wizara hiyo na kuzungumza nao namna bora ya utekelezaji wa majukumu ya Wizara ili kusukuma kasi ya maendeleo ya uchumi wa Taifa. 

Akizungumza katika kikao hicho Dkt. Mpango alisema Wizara ya Fedha na Mipango ni kitovu cha Serikali hivyo Watumishi wote wa Wizara wanawajibu wa kutekeleza majukumu kwa kuzingatia nidhamu, maadili, sheria, kanuni na taratibu za utumishi wa Umma ili kuongeza tija. 

Amesema kila mtumishi anawajibu wa kufanya kazi kwa weledi, bidii na kushirikiana na kila mmoja katika nafasi yake ili kuboresha utendaji kazi na kukuza uhusiano mahala pa kazi.

Aidha Waziri Mpango aliwapongeza Watumishi wa Wizara hiyo kwa kazi wanazozifanya hususan kazi ya uandaaji wa Bajeti Kuu ya Serikali, Uchambuzi wa Sera za Taifa na uanzishwaji wa mfumo mpya wa ukusanyaji wa mapato ya Serikali kwa njia ya Kielektroniki-GePG.

Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Khatibu Kazungu amemhakikishia Waziri Mpango kuwa watatekeleza maelekezo yote aliyoyatoa kwa ukamilifu ili kuboresha utendaji kazi wa Wizara hiyo.

No comments:

Post a Comment

Pages