Mkuu wa Uhusiano wa MultiChoice Tanzania Johnson Mshana akimkabidhi mshindi wa tuzo za kimataifa za DStv Eutelsat Star Awards Pricilla Marealle cheti cha ushindi wakati wa mahafali ya kidato cha sita katika shule ya St Mary Goretti hivi karibuni. Kulia ni Afisa Uhusiano wa MultiChoice Tanzania. Grace Mgaya. Pricilla aliibuka mshindi wa kwanza katika tuzo hizo na kuwashinda wanafunzi kutoka nchi zaidi ya 10 kote barani Afrika. Mbali na kutunukiwa cheti maalum, Pricilla atapata fursa ya kutembelea kituo cha Anga cha Afrika Kusini na makao makuu ya MultiChoice jijini Johannesburg.
Mkuu wa Shule ya St Mary Goretti Sr. Lucrecia Njau
akifurahi baada ya kupokea cheti kutoka kwa Mkuu wa Uhusiano wa
MultiChoice Tanzania Johnson Mshana mara baada ya shule hiyo kufanikiwa
kutoa mshindi wa jumla wa wa tuzo za kimataifa za DStv Eutelsat Star
Awards Pricilla Marealle. Pricilla aliibuka mshindi wa kwanza katika
tuzo hizo na kuwashinda wanafunzi kutoka nchi zaidi ya 10 kote barani
Afrika. Mbali na kutunukiwa cheti maalum, Pricilla atapata fursa ya
kutembelea kituo cha Anga cha Afrika Kusini na makao makuu ya
MultiChoice jijini Johannesburg
Mshindi wa Jumla wa tuzo za kimataifa za DStv
Eutelsat Star Awards Pricilla Marealle akikabidhiwa kikombe cha ushindi
na Mkuu wa shule ya St Mary Goretti Sr. Lucrecia Njau baada ya
kutangazwa kuwa mshindi wa jumla wa wa tuzo za kimataifa za DStv
Eutelsat Star Awards. Kulia ni Mkuu wa Uhusiano wa MultiChoice Tanzania
Johnson Mshana. Pricilla aliibuka mshindi wa kwanza katika tuzo hizo na
kuwashinda wanafunzi kutoka nchi zaidi ya 10 kote barani Afrika. Mbali
na kutunukiwa cheti maalum, Pricilla atapata fursa ya kutembelea kituo
cha Anga cha Afrika Kusini na makao makuu ya MultiChoice jijini
Johannesburg.
Mshindi wa Jumla wa tuzo za kimataifa za DStv Eutelsat
Star Awards Pricilla Marealle akifurahi na wazazi wake Calvin Marealle
na Jamila Marealle mara baada ya kukabidhiwa cheti cha ushindi. Pricilla
aliibuka mshindi wa kwanza katika tuzo hizo na kuwashinda wanafunzi
kutoka nchi zaidi ya 10 kote barani Afrika. Mbali na kutunukiwa cheti
maalum, Pricilla atapata fursa ya kutembelea kituo cha Anga cha Afrika
Kusini na makao makuu ya MultiChoice jijini Johannesburg.
Mkuu wa Uhusiano wa MultiChoice Tanzania Johnson Mshana
(Kulia) na Afisa Uhusiano wa kampuni hiyo Grace Mgaya (kushoto)
wakikabidhi seti ya DStv kwa mkuu wa shule ya sekondari St Mary Goretti
Sr. Lucrecia Njau na mshindi wa tuzo za kimataifa za DStv Eutelsat Star
Awards Pricilla Marealle wakati wa mahafali ya kidato cha sita katika
shule ya St Mary Goretti hivi karibuni. Pricilla aliibuka mshindi wa
kwanza katika tuzo hizo na kuwashinda wanafunzi kutoka nchi zaidi ya 10
kote barani Afrika. Mbali na kutunukiwa cheti maalum, Pricilla atapata
fursa ya kutembelea kituo cha Anga cha Afrika Kusini na makao makuu ya
MultiChoice jijini Johannesburg wakati shule yake imepata cheti na
zawadi ya kufungiwa huduma ya DStv.
Na Mwandishi Wetu
KWA mara nyingine tena Tanzania imeibuka kinara katika tuzo za kimataifa za wanafunzi zijulikanazo kama DStv Eutelsat Star Awards ambapo mwanafunzi Priscilla Marealle kutoka shule ya sekondari ya St. Mary Goreti mkoani Kilimanjaro ameweza kuipeperusha bendera ya Tanzania kwa kunyakua nafasi ya kwanza katika kipengele cha uchoraji bango ikiwa ni baada ya mchuano mkali baina ya mamia ya wanafunzi kutoka nchi zaidi ya 10 kote barani Afrika.
Kwa upande wa uandishi wa insha kijana
Tanaka Chonyera kutoka nchini Botswana aliweza kujinyakulia ushindi wa kwanza.
Tuzo
hizi ambazo huhusisha uandishi wa insha maalum au kuandaa bango yenye
ujumbe kuhusiana na elimu ya anga hususan Setelait
ni za wazi kwa wanafunzi wote wa shule za sekondari wenye umri kati ya
miaka 14 – 19 kote barani Afrika ambapo kampuni ya MultiChoice
inaendesha shughuli zake.
Katika msimu huu wa nane, washindani walitakiwa kuandika insha au kubuni bango litakaloelezea licha ya Satelait kutumika
katika shughuli mbalimbali, ni namna gani zitaweza kutumika zaidi ili kuleta maendeleo chanya ulimwenguni.
Priscilla
ambaye ni mwanafunzi wa kidato cha sita wa mchepuo wa Sayansi katika
shule ya Mtakatifu Maria Goreti alitangazwa
rasmi kuwa mshindi mjini Accra nchini Ghana ambapo ndipo jopo la
watahini liliongozwa na Paolo Nespoli, mwanaanga nguli kutoka European
Space Agency (ESA) lilikaa kupitia kazi kutoka kwa wanafunzi walioshinda
katika nchi mbalimbali.
Akiongea
baada ya kukabidhiwa cheti cha uthibitisho wa ushindi wakati wa
mahafali ya kidato cha sita ya shule ya Mtakatifu
Mary Goreti iliyopo Moshi Kilimanjaro, Priscilla amesema amefurahi sana
kwa ushindi huo mkubwa ambao umemletea yeye, shule yake na taifa zima
kwa ujumla sifa kubwa. “Nimefurahi sana kupokea taarifa hizi nzuri.
Naamini ushindi wangu utakuwa ni chachu kubwa
kwa wanafunzi wenzangu kote nchini kujitokeza kwa wingi na kushiriki
katika tuzo kama hizi na mashindano mengine ya kitaaluma ya ndani na nje
ya nchi, na kusisitiza kuwa Ndoto huanza kufanya kazi pale
unapojiamini” alisema Priscilla.
Kwa
upande wake mkuu wa shule hiyo ya Mtakatifu Maria Goreti Sister
Lucresia Njau alisema kuwa anaishukuru sana kampuni
ya MultiChoice Tanzania kwa kuwapatia nafasi ya kushiriki katika
Mashindano hayo na hatimaye kuweza kunyakua tuzo hiyo kupitia mwanafunzi
wao Priscilla.
“Huyu
kijana ana jitahidi sana katika chochote kile anachokifanya, iwe ni
darasani au hata katika majukumu mengine nje ya darasani. Ni msikivu
mtiifu lakini zaidi ya yote ni mbunifu
sana. Naamini haya ndiyo yaliyomfanya aweze kushinda tuzo hizi” alisema
Sr. Lucrecia Njau.
Naye,
Mkuu wa Uhusiano MultiChoice Tanzania Johnson Mshana alisema,” Huu ni
msimu wa tatu mfululizo kwa Tanzania kuendelea
kung’ara katika tuzo hizi za DStv Star Awards. Tulianza kupeperusha
bendera yetu na kijana Davids Bwana msimu wa sita baada ya kushika
nafasi ya pili Afrika katika kipengele cha uandishi wa insha, kisha
tukaibuka kidedea baada ya kupokea taarifa za ushindi
wa kwanza wa kijana Taheer Rashid katika msimu wa saba mwaka jana na
leo hii tunayofuraha kubwa kuona kuwa tumeendeleza wimbi la ushindi.”
Wakizungumza
kwa nyakati tofauti baada ya Pricilla kutangazwa kuwa mshindi, walimu
na wazazi wa mwanafunzi huyo wa kidato cha sita mwenye umri wa miaka 19,
wamesema kuwa wanamfahamu
vyoma Pricilla kuwa ni kijana mwenye kupenda kujibidisha sana katika
masuala ya kitaaluma na kijamii hivyo ushindi wake ni kitu
kilichotarajiwa na kwamba wanaamini kuwa anastahili ushindi huo.
Pamoja na kupata cheti
maalum cha ushindi, Pricilla atapata fursa (Yeye na Mzazi au mlezi) ya
kutembelea kitua cha Anga cha Afrika Kusini na pia kutembelea makao
makuu ya MultiChoice jijini
Johannesburg kama mgeni maalum wa DStv huku shule aliyotoka ikipata
zawadi ya cheti pamoja na kufungiwa huduma ya DStv.
No comments:
Post a Comment