NA MWANDISHI WETU
KAMPUNI
ya Total Tanzania Limited, imetoa Sh. Mil. 65 kwa vijana wa Kitanzania
watatu baada ya kuibuka washindi wa shindano la kuandika mradi wa
kijasiriamali lilizoanza Oktoba mwaka 2018.
Hayo
yamesemwa na Mkurugenzi Mkuu wa Total Tanzania Ltd, Tarik Moufaddal
wakati akitoa taarifa kwa mgeni rasmi Naibu Waziri wa Kazi, Ajira na
Vijana, Anthony Mavunde katika hafla ya kuwazawadia washindi fedha hizo
iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi
huyo alisema ili kupatikana kwa washindi hao watatu walipokea zaidi ya
maandiko 600 ya miradi ya ujasiriamali ambapo majaji walipitia na
kubakiza 100, 15 hadi watatu ambao wametangazwa jana.
Moufaddal
alisema mwitikio ulioneshwa na vijana katika shindano hilo
kijasiriamali umewapa mwamko wa kuendelea nalo kwa miaka ijayo.
"Mradi
wa shindano la kijasiriamali umekuwa na manufaa ambapo zaidi ya maombi
600 yalipokelewa na jana tumepata washindi watatu ambapo wamefanikiwa
kupata shilingi milioni 65," alisema.
Mkurugenzi
huyo alisema mshindi kwanza ni Doreen Noni ambaye amepata Sh.Mil 30,
Sai Michale mshindi wa pili Sh.Mil 20 na Prince Tilya mshindi wa tatu
Sh.Mil.15.
Kwa upande
wake Mkurugenzi wa Sheria na Mahusiano Total Tanzania Marsha Msuya
alisema Sh.Mil 200 zimetumika kufanikisha shindano hilo.
Alisema
pamoja na washindi kupatikana bado Total Tanzania Ltd itatumia zaidi ya
milioni 20 kwa ajili ya kugharamia mafunzo kwa kipindi cha miezi mitatu
kwa washindi.
"Sisi
tumejipanga kushirikiana na Serikaki katika kuinua jamii ya Watanzania
na shindano hili ni sehemu ya mchango wetu kwa jamii kwani tumesaidia
ujenzi wa madarasa, vyoo na kutoa elimu ya usalama barabarani," alisema.
Akizungumzia
shindano hilo la kijasiriamali, Naibu Waziri Mavunde alisema ni la
kuigwa na wadau wengine ili kuounguza adha ya ukosefu wa ajira.
Mavunde alisema Watanzania wengi wanahitaji ajira na kujiajiri hivyo walichofanya Total ni jambo zuri la kuigwa na kuendelezwa.
"Tafiti zinaonesha zaidi ya Watanzania milioni 22.3 wanaweza kufanya kazi ambapo wengi ni kundi la miaka 15 na kuendelea.
Tafiti
hiyo inaonesha katika idadi hiyo wenye ujuzi wa juu ni asilimia 3.6,
16.9 ujuzi wa kati na 79.6 ujuzi wa chini hivyo bado elimu ya ujuzi
inahitajika," alisema.
Naibu
Waziri alisema serikali imejipanga kikamilifu kutoa elimu ya ujuzi kwa
Watanzania milioni 4.4 ifikapo 2021 huku malengo makubwa yakielekezwa
kwa vijana.
Alisema pia
serikali imejipanga kufikia wananchi 18,500 katika mikoa 12 kuwapatia
elimu ya kilimo kitalu nyumba ili kuongeza ajira.
Mavunde
alisema atahakikisha washiriki waliofika 15 bora mawazo yao
yanachukuliwa na kuendeleza na kuipongeza Total Tanzania Ltd kwa
uthubutu waliouonesha kuwezesha vijana.
Mshindi
wa kwanza Noni ambaye aliwasilisha wazo la kijasiriamali lenye lengo la
kuelkmisha jamii namna ya kukabiliana na msongo wa mawazo alisema
atatumia fedha hizo kubadilisha jamii ya kitanzani kwa kuilimisha.
Alisema vijana wengi wanakabiliana na changamoto ila wamekosa watu wa karibu wa kujadiliana nao namna ya kupambana na hali hiyo
No comments:
Post a Comment