Meneja Mikopo kwa Wajasiriamali Wanawake wa Benki ya CRDB, Rehema Shambwe, akiwasili katika mkutano uliondaliwa kwa ajili ya kuwawezesha wanawake kwenye Uwekezaji wa Soko la Mitaji na Dhamana.
Ofisa Mahusiano ya Wateja, Idara ya Hazina na Masoko ya Mitaji Benki ya CRDB, Mary Mponda, akitoa mada katika mkutano wa mkutano ulioandaliwa na benki hiyo kwa ajili ya kuwawezesha wanawake kwenye Uwekezaji wa Soko la Mitaji na Dhamana.
Msimamizi Mikopo ya Kwenye Kadi, Stanley Methe, akizungumza katika mkutano huo.
Meneja Mwandamizi Idara ya Hazina na Masoko ya Mitaji wa Benki ya CRDB, Fredrick Siwale, akizungumza katika mkutano huo.
MC wa mkutano huo akizungumza jambo.
Baadhi ya washiriki wa mkutano huo.
Ofisa Mahusiano ya Wateja, Idara ya Hazina na Masoko ya Mitaji Benki ya CRDB, Mary Mponda, akitoa mada katika mkutano wa mkutano ulioandaliwa na benki hiyo kwa ajili ya kuwawezesha wanawake kwenye Uwekezaji wa Soko la Mitaji na Dhamana.
Msimamizi Mikopo ya Kwenye Kadi, Stanley Methe, akizungumza katika mkutano huo.
Meneja Mwandamizi Idara ya Hazina na Masoko ya Mitaji wa Benki ya CRDB, Fredrick Siwale, akizungumza katika mkutano huo.
MC wa mkutano huo akizungumza jambo.
Baadhi ya washiriki wa mkutano huo.
Baadhi ya washiriki wa mkutano huo wakisikiliza mada zilikuwa zikiwasilishwa.
Mkuu wa Kitengo cha Huduma ya Uwekezaji katika Masoko ya Mitaji Benki ya CRDB, Masumai Hemed, akizungumza katika mkutano huo.
Washiriki.
Baadhi ya washiriki.
Mkutano ukiendelea.
Baadhi ya akinamama wakipata chai baada ya mkutano.
Mkuu wa Kitengo cha Masoko Kampuni ya Solomon Stock Brokers, Mariam Solomon, akizungumza katika mkutano.
Mshiriki akiuliza swali.
Mkutano ukiendelea.
Mkurugenzi wa Uwekezaji wa Benki ya CRDB, Hilda Rweshane, akizungumza wakati wa kufunga mkutano ulioandaliwa na benki hiyo kwa ajili ya kuwawezesha wanawake kwenye Uwekezaji wa Soko la Mitaji na Dhamana uliofanyika jijini Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki.
Mkutano ukiendelea.
Mkurugenzi wa Uwekezaji wa Benki ya CRDB, Hilda Rweshane, akizungumza wakati wa kufunga mkutano ulioandaliwa na benki hiyo kwa ajili ya kuwawezesha wanawake kwenye Uwekezaji wa Soko la Mitaji na Dhamana uliofanyika jijini Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki.
NA JOHN MARWA
WANAWAKE wameombwa kutumia huduma za uwekezaji salama ‘Custodial Services’ ambao inatolewa na Benki ya CRDB kwa gharama nafuu ambazo humsaidia mwekezaji anayewekeza kwenye masoko ya mitaji kulinda amana zake, kupata taarifa za uwekezaji wake pamoja na magawio yake kirahisi zaidi.
Huduma hiyo humsaidia mteja kupata taarifa katika soko la ndani na masako ya Afrika Mashariki ambayo huwasaidia kuongeza thamani ya uwekezaji wao pamoja na kuweka taarifa na kumbukumbu zao ambazo huwasaidia wakati wa uhai wao na hata pindi wanapokuwa wamefariki pia huwarahishia warithi wao kupata haki yao kirahisi zaidi.
Mkutano huo uliandaliwa na benki hiyo, ulifanyika jijini Dar es Salaam, ikiwa ni muendelezo wa maadhimisho ya siku ya Wanawake yanayofanyika kila mwaka Machi nane.
Akizungumza wakati wa kufungua Mkutano huo, Mkuu wa Kitengo cha Huduma ya Uwekezaji katika Masoko ya Mitaji Benki ya CRDB, Masumai Hemed, alisema wanawake wanapaswa kuchangamkia fursa hizo ili kujiimarisha kiuchumi.
Akitoa elimu ya jinsi mfumo huo unavyofanya kazi Ofisa Mahusiano ya Wateja, Idara ya Hazina na Masoko ya Mitaji Benki ya CRDB, Mary Mponda, aliwaomba Wamama kujiunga na mfumo wa mauzo na manunuzi kwani ni mfumo salama wa uwekezaji unaomuwezesha mteja kutengeneza faida wenye usalama wa pesa zake.
“Ukijiunga na mfumo huu taarifa za uwekezaji wako zinakuwa kwenye usimamizi wa kimfumo, pia inamsaidia mteja kujua nguvu ya uwekezaji wake kutokana na hali ya soko la hisa, lakini pia mteja akiwa chini ya mfumo huu anaweza kununua hisa katika masoko ya hisa ya nchi za Afrika Mashariki.
“Pia unatoa ripoti za kila wiki za mwenendo wa masoko yote ya hisa tunayofanya nayo kazi hali ambayo humsaidia mteja kujua ni wapi pa kuwekeza kwa wakati ili kutengeneza faida hasa pale soko la ndani linapoyumba,”alisema Mponda na kuongeza kuwa.
“Mfumo huo unampa mteja nafasi ya kuchukua mkopo wenye riba ya asilimia 0.2 kwa mwaka kulingana na kiasi alichowekeza,”alisema.
Akifunga Mkutano huo Mkurugenzi wa Uwekezaji wa Benki ya CRDB, Hilda Rweshane, aliwataka Wanawake kutumia vema fursa wanazozipata katika uwekezaji ili kujikwamua kimaisha kwani wana fursa pana katika jamii wanayoishi.
Rweshane alisema wanawake ni wawekezaji wazuri kama watatumia vema fursa waliyonayo katika familia, jamii na taifa kwa ujumla kwa kuzingatia nafasi yao na nini wanapaswa kukifanya katika ngazi zote za uzalishaji.
“Sisi Wamama ni wawezakezaji wazuri kama tutatumia vizuri fursa tuliyonayo katika Jamie, tutekeleze majukumu yetu katika ngazi ya familia kama wamama lakini pia tutumie fursa zinazo tuwezesha kuyatekeleza hayo kwa kuendelea kuwa wawekezaji ili kujiongezea kipato.
“Tusikubali pesa itutumikishe bali inapaswa kututumikia sisi, kwa kufanya shughuli ambazo zinatupatia muda wa kutosha kutekeleza majukumu yetu kama wanawake. Niwaombe sana tuzingatie taarifa hizi tulizozipata hapa, uzuri wa kitu ukipata taarifa zake zitumie katika kupinga hatua nyingine,”alisema Rweshane.
Aidha aliwataka wamama kuwasaidia watoto wao kujua thamani ya kuwekeza wangali wadogo ili kuondokana na utegemezi pale wazazi wao wanapoondoka.
No comments:
Post a Comment