Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako akizungumza na wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii (Hawapo Pichani) walipofanya ziara katika Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere kukagua mradi wa upanuzi na ukarabati wa Chuo hicho.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof.
Joyce Ndalichako na Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Wiliam Ole
Nasha akijadiliana jambo katika kikao na wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge
ya Huduma na Maendeleo ya Jamii (Hawapo Pichani) walipofanya ziara katika Chuo
cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere kukagua mradi wa upanuzi na ukarabati wa Chuo
hicho.
Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu
Nyerere Stephen Wasira akitoa maelezo kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma
na Maendeleo ya Jamii (Hawapo Pichani) walipofanya ziara katika Chuo cha
Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere kukagua mradi wa upanuzi na ukarabati wa Chuo
hicho.
Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia
William Ole Nasha akiongoza wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na
Maendeleo ya Jamii wakati wa kukagua maendeleo ya ujenzi wa ukumbi wa kisasa wa
Mihadhara unaojengwa kwa mapato ya ndani ya Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu
Nyerere.
Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya
Huduma na Maendeleo ya Jamii wakikagua ukumbi mpya wa mihadhara wa Chuo cha
Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere uliyojengwa kwa fedha zinazotokana na mapato ya
ndani za chuo hicho.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako, akiwaongoza Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii wakati wakikagua ukumbi mpya wa mihadhara wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
Dar es Salaam, Tanzania
Kamati ya Bunge ya
Kudumu ya Huduma na Maendeleo ya Jamii imekamilisha ziara ya kukagua
utekelezaji wa Miradi mitatu mikubwa inayogharimiwa na Serikali kupitia bajeti
ya Mwaka 2018/19 katika baadhi ya Vyuo vilivyo chini ya Wizara ya Elimu ,
Sayansi na Teknolojia na kuridhishwa na utekelezaji wa Miradi hiyo.
Kamati hiyo
imetembelea Chuo Kikuu kishiriki cha Elimu (DUCE) katika mradi wa upanuzi na
ukarabati wa jengo la Utawala ambalo linagharimu shilingi Bilioni 3.2 ambapo kazi hiyo inaendelea na
litakapo kamilika litaongeza nafasi kwa ajili ya ofisi za watumishi na vyumba
vya mikutano.
Aidha kamati
imetembelea mradi wa upanuzi wa vyumba vya mihadhara katika Chuo Kikuu Ardhi
kazi ambayo imekamilika kwa hatua ya kwanza na itagharimu
shilingi Bilioni 2.5 hadi kukamilika
kwake.
Kamati imekamilisha
ziara yake katika Chuo Cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere, ambapo Wajumbe
watembelea Jengo la jipya la Mihadhara linalojengwa kwa mapato ya ndani ya Chuo
hicho, ambalo linauwezo wa kuchukua wanafunzi zaidi ya 300 kwa wakati
mmoja. Aidha kamati imepongeza wizara na
uongozi wa Chuo kwa kazi nzuri na kubwa iliyofanyika katika kusimamia ujenzi
huo. Jengo hilo limekamilika kwa asilimia 95.
Aidha
Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Mh. Prof. Joyce Ndalichako
amepongeza uongozi wa Chuo kwa kusimamia vema matumizi ya fedha za zinazotokana
na Mapato ya ndani na kutumika kwa kutekeleza miradi yenye tija kwa Chuo. Ametumia nafasi hiyo kumpongeza
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh John Pombe Magufuli kwa kusimamia
suala la kubana matumizi na kuelekeza fedha katika kazi zenye faida kwa jamii
kama ilivyo kwa Chuo Cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere.
Katika majumuisho ya
ziara hiyo, Kaimu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma
na Maendeleo ya Jamii Mh. Oscar
Mukasa (Mb) ameipongeza wizara na taasisi zilizotembelewa kwa kusimamia
utekelezaji wa miradi na kushauri taasisi hizo kujikita katika kusimamia Dira
na dhima za uanzishwaji wake. Kamati pia imeshauri Serikali kupitia Wizara
kuhahakisha inatoa fedha za miradi kwa wakati kulingana na bajeti.
Imetolewa na:
Kitengo Cha Mawasiliano Serikalini,
WIZARA YA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA
18/3/2019
Kitengo Cha Mawasiliano Serikalini,
WIZARA YA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA
18/3/2019
No comments:
Post a Comment