Mhadhiri wa Chuo Kikuu Mzumbe, Emmanuel Akili, akitoa mada katika semina ya kuwajengea uwezo wataalamu kutoka taasisi mbalimbali katika masuala ya maendeleo ya uchumi katika sekta ya usafiri na usafirishaji mijini. Semina hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam chini ya Chuo Kikuu Mzumbe kwa kushirikiana na taasisi ya Kuehne. (Picha na Francis Dande).
Mhadhiri wa Chuo Kikuu Mzumbe, Emmanuel Akili, akitoa mada katika semina hiyo.
Baadhi ya washiriki wa semina hiyo.
Mhadhiri wa Chuo Kikuu Mzumbe, Emmanuel Akili, akitoa mada katika semina hiyo.
Baadhi ya washiriki wa semina hiyo.
NA JOHN MARWA
CHUO Kikuu Mzumbe kwa kushirikiana na Taasisi ya
Kuehne ya nchini Uswis wameendesha Semina kwa wataalamu juu ya kuwajengea uwezo
wa masuala ya kimkakati wa maendeleo ya uchumi katika sekta ya usafiri na
usafirishaji mijini.
Semina hiyo ya siku tatu ilifunguliwa jana katika
kampusi ya chuo hicho jijini Dar es Salaam na kushirikisha wataalamu kutoka
Taasisi mbalimbali katika kujengewa uwezo.
Kwamba, baada ya semina hiyo wahusika
watakwenda kutoa elimu na kujenga mikakati ya kutatuia changamoto za sekta ya
usafiri na usafirishaji katika miji na majiji nchini.
Akizungumzia na Habari Mseto Mratibu wa semina hiyo,
Dk. Omary Swalleh amesema dhima ya semina hiyo ni kuwajengea watalamu uwezo kwa
ajili ya kuipeleka nchi mbele katika maendeleo ya kiuchumi kupitia sekta ya
usafiri na usafirishaji.
“Chuo Kikuu Mzumbe kwa kushirikiana na taasisi ya
Kuehne kupitia kampuni yake ya KUEHNE, hii tasisi inatusapoti sisi ili
kuwajengea wataalamu uwezo kwa ajili ya kuipeleka nchi mbele kwa kutatua
changamoto mbali mbali za kimaendeleo.
“Huyu mtu anaitwa Kuehne ni moja ya watu tajiri na
ameendelea kupitia mipango mkakati ya usafirishaji, Tasisi hi inashirikiana na
vyuo mbali mbali barani Afrika,” amesema na kuongeza:
“Nchi hizo ni Kenya, Rwanda, Nigeria, Seaneger na
Seala Leon na Tanzania kupitia Chuo Kikuu Mzumbe na Chuo Kikuu cha
Dar es Salaam ndio vimepata bahati ya kushirikiana na tasisi hii, hapa nchini
”alisema na kuongeza kuwa.
“Fursa hii kwetu ni changamoto na inatusaidia pia
kuwaita wataalamu wetu kama hao na leo unavyoona kuna semina ambayo inahusu endeshaji
wa sekta ya usafiri na usafirishaji mijini ili tuone namna gani
inaweza kusaidia katika maendelea ya uchumi hapa Tanzania.
“Tunaamini kama sekta ya usafiri na usafirishaji
itakwenda vizuri basi mchango wake kwenye uchumi ni mkubwa kwa maana watu watafika
sehemu moja kwa wakati, vitu vitafika kwa na hiyo itaweza kukuza uchumi wa nchi
kwa wakati.
Ameongeza, wao kama taasisi wanaamini kuwa kwa
kuendesha semina hasa kwa wataalamu wa makapuni na mashirika wataweza kuweka
mikakati ya kuboresha sekta ya usafiri na usafirishaji kwa kila mmoja kutimiza
wajibu wake basi sekta hiyo itakuwa imara na kuwa kitovu cha uchumi.
“Maswala ya usafiri na usafirisahji yanshirikisha
tasisi mbali mbali, madereva wanawajibu wao, trafic wanawajibu wao sumatra
wanawajibu wao cha msingi ni kila mtu kutimiza wajibu wake na sisi mchango wetu
ni kuwajengea uwezo waweze kutimiza majukumu yao,”amesema.
No comments:
Post a Comment