Shomari Kapombe |
NA JOHN MARWA
BEKI matata wa klabu ya Simba na timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars,
Shomari Kapombe, ameimwagia Timu ya Taifa kongore na kueleza kuwa hali yake
inaendelea vizuri kwa sasa.
Kapombe aliumia mguu kwa kuvunjika mfupa wa ndani huko Afrika Kusini wakati kikosi cha Stars kilipokuwa kimeweka kambi maalum kujiandaa na mechi za kuwania kufuzu AFCON dhidi ya Lesotho.
Baada ya matibabu kukamilika Kapombe ameeleza kwa sasa maendeleo yake ni mazuri na tayari ameshaanza mazoezi mepesi nje ya uwanja huku akisema anatarajia kuanza kujifua na timu yake ya Simba mwishoni mwa mwezi huu.
"Namshukuru Mungu hali yangu kwa sasa inaendelea vizuri.
"Natarajia kuanza mazoezi mepesi na wachezaji wenzangu mwishoni mwa mwezi huu.
Kuhusu Taifa Stars kufuzu kuingia kwenye mashindano ya AFCON mwaka huu yatakayofanyika huko Misri kwa kuifunga Uganda mabao 3-0 kwenye Uwanja wa Taifa, Kapombe amesema amefururahishwa na matoke ohayo na kuwapongeza nyota wa stars kwa kazi nzuri waliyoifanya.
"Nimefurahi sana kama mtanzania ambaye pia nilikuwa kwenye kikosi huko nyuma licha ya kutolewa baadaye kwakuwa nisingeweza kucheza.
"Natoa pongezi kubwa kwa wachezaji wenzangu, na wale waliosaidia kufika hatua hii.
"Ni jambo kubwa sana kutokea kwasababu ni miaka 39 nafasi hii ilikuwa haijatokea kwetu, nina furaha kubwa kwakweli".
No comments:
Post a Comment