NA FRANCIS DANDE
MULTCHOICE Tanzania imetangaza fursa ya kipekee kwa
wadau wa tasnia ya filamu Tanzania na barani Afrika ijulikanayo kama MultiChoice
Talent Factory Portal iliyodhamiria kuleta mapinduzi ya hali ya juu katika uandaaji
wa filamu zenye viwango vya Kimataifa.
Akizungumza
wakati wa uzinduzi wa programu hiyo, Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano wa MultiChoice
Tanzania, Johnson Mshana alisema programu hiyo ni muendelezo wa program maalum iliyodhamiria
kuleta mabadiliko katika tasnia ya filamu barani Afrika.
“MultiChoice
Talent Factory ambayo ni program mama ilizinduliwa rasmi Mei mwaka jana na
imedhamiria kuleta mabadiliko chanya kwenye tasnia ya filamu hapa nyumbani Tanzania
na Afrika kwa ujumla. Tulianza kwa kupeleka vijana wanne katika kambi maalum ya
mafunzo ya uandaaji filamu katika akademia maalum Nairobi Kenya, kisha mafunzo maalum
kwa magwiji wa sauti yaliyofanyika Januari mwaka huu na hatimaye leo hii
tumekuja tena na platform maalum yenye dhamira ile ile ya kuleta mapinduzi
katika tasnia ya filamu barani Afrika,” alisema Mshana.
Katibu
Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania, Joyce Fisoo anaishukuru MultiChoice kwani
imekuwa mstari wa mbele kuleta mapinduzi kwenye filamu hapa nyumbani Tanzania. alishuhudia uzinduzi wa programu ya
MultiChoice Talent Factory mapema mwaka jana kule mjini Dodoma na leo hii tunazindua
tena sehemu nyingine ya programu hiyo hiyo.
Fisoo
alisema hakika ni fursa ya kipekee na ninapenda kuchukua nafasi hii
kuwahamasisha wadau wote waliopo katika Tasnia yetu kuitumia nafasi hii
ipasavyo ili kuweza kujifunza, kubadilishana ujuzi na hatimaye kupata kazi
zenye maudhui ya hali ya juu kutoka hapa hapa Afrika.
Naye Ofisa
Uhusiano wa MultiChoice Tanzania, Grace Mgaya alimalizia kwa kueleza kuwa ukurasa
huu ni wa wazi kwa watu wote hususani wadau wa filamu waliopo hapa nchini na
Afrika kwa ujumla.
No comments:
Post a Comment