Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, akisalimiana na Maofisa Habari na Mawasiliano Serikalini wakati alipowasili kwenye Ukumbi wa Benki Kuu jijini Mwanza jana, kufungua mkutano wa Kazi wa Siku Tano wa Maofisa hao. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Mwanza, Tanzania
WAZIRI
MKUU, Kassim Majaliwa amewataka Maafisa Habari, Uhusiano na Mawasiliano
Serikaliniwajitathmini kwa kina zaidi kuhusu namna walivyotekeleza
wajibu wao na watafakari njia bora ya kuyatangaza na kuyatetea mafanikio
ya mageuzi makubwa yanayoendelea nchini.
Pia,
amewataka Maafisa Habari, Uhusiano na Mawasiliano Serikaliniwahakikishe
wanatumia vizuri taaluma zao na nyezo wanazopatiwa kusema mambo
yanayofanywa kwenye sekta zote na wasipofanya hivyo watatoa fursa kwa
taarifa zinazosemwa na wapinga maendeleo kuonekana kuwa ni kweli.
Waziri Mkuu ameyasema hayo leo (Jumatatu, Machi 18, 2019)katika
ufunguzi wa Kikao Kazi cha 15 cha Maafisa Habari, Uhusiano na
Mawasiliano Serikalini, kinachofanyika katika ukumbi wa BOT jijini
Mwanza. Kikao hicho kinahudhuriwa na Maafisa Habari na Mawasiliano
takbaribani 400.
Amesema
maafisa hao wanatakiwa wakumbuke kuwa wanapaswa kuueleza umma wa
Watanzania kwa kina masuala yanayofanywa na Serikali hususan katika
kipindi hiki ambacho Serikali inatekeleza Mpango wa Pili wa Maendeleo wa
Miaka Mitano (2016/2017 – 2020/2021) wenye kuweka msisitizo kwenye
ujenzi wa uchumi wa viwanda.
“Mkumbuke
kuwa kazi ya utoaji taarifa kwa wananchi kwa sasa si utashi binafsi wa
mtoa habari bali hainabudi kufanywa kwa mujibu wa sheria na katiba ya
nchi. Mathalan Sheria mpya ya Haki ya Kupata Taarifa Na. 12 ya mwaka
2016 yenye kuzitaka mamlaka za umma kuwapa wananchi taarifa
zinazowahusu”.
Waziri
Mkuu amesema sheria hiyo, inakwenda sambamba na sheria nyingine ya
kumlinda mwananchi asilishwe taarifa za uongo, uchochezi na uzushi yaani
Sheria ya Huduma za Habari Na. 12 ya mwaka 2016.
Amesema
lengo la katiba na sheria hizo mbili, pamoja na mambo mengine, ni
kuwahakikishia wananchi haki ya kupata habari tena zilizothibitishwa kwa
maana ya usahihi wake na kwa wakati. “Sababu hizo, ndizo zilizofanya
niguswe sana na kauli mbiu yenu isemayo: “utoaji habari sahihi na kwa
wakati ni chachu katika kuifikia Tanzania ya kipato cha kati”.
Pia,
Waziri Mkuu ametumia fursa hiyo kupongeza kazi nzuri zinazofanywa na
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais Ikulu, Wizara ya Habari, Utamaduni,
Sanaa na Michezo (hususan Idara yake ya Habari - MAELEZO) na timu za
habari za viongozi wakuu kama Mawaziri, Wakuu wa Mikoa na watendaji
wengine.
Pia,
Waziri Mkuu amesema ameguswa na baadhi ya mada ambazo zitajadiliwa
katika kikao kazi hiko, ikiwemo ya namna ya kushughulikia habari
za uongo, kutunga, kughushi na namna kada yao inavyoweza kusaidia
kukidhibiti kichochoro hicho haramu katika habari.
Kadhalika,
Waziri Mkuu amewataka viongozi na watendaji wote wa taasisi za umma,
kuanzia sasa washirikiane na maafisa wa habari kwenye maeneo yao
kuhakikisha kuwa habari muhimu kwa wananchi hazizuiwi kwa urasimu kama
hazijazuiwa kisheria. Habari zitolewe kwa haraka na kwa njia anuai za
kisasa.
Waziri
Mkuu amemuagiza Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dkt.
Harrison Mwakyembe afuatilie kuhusu uzinduzi wa tovuti za Halmashauri
walioufanya jijini Dodoma tarehe 27 Machi 2017, kama zinafanya kazi
ipasavyo.
Amesema
lengo la tovuti hizo ni kuiongezea Serikali uwezo wa kuwapatia wananchi
habari na taarifa kwa haraka kwa kuzingatia kwamba wako katika kipindi
muhimu cha mageuzi katika historia ya nchi, ambapo mambo mengi
yanafanyika Serikalini ya kiuchumi na kijamii lakini hayafikishwi kwa
wananchi.
“Kuhusu
hili, naiagiza Wizara ya Habari kufanya tathmini ya mara kwa mara na
kuniletea taarifa kuhusu utekelezaji wa majukumu yenu na matakwa haya ya
kisheria miongoni mwa wizara, taasisi za umma na sekretarieti za mikoa
na Halmashauri mbalimbali nchini”.
Waziri
Mkuu amesema maafisa hao wanapaswa kufahamu kikao chao kimekuja wakati
muafaka kwani Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt. John
Magufuli, ipo katika mwaka wake wa nne wa kutekeleza mageuzi makubwa
katika kila sekta zikiwemo za kiuchumi na kijamii nchini.
Amesema
katika kipindi cha zaidi ya miaka mitatu kazi kubwa tena ya kihistoria
imefanywa na Serikali ya awamu ya tano na wao ni mashahidi wa hayo
yanayofanywa. “Ni jukumu lenu sasa kuuhabarisha umma wa Watanzania kama
ambavyo Katiba yetu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inavyotaka katika
Ibara ya 18(d).
Waziri Mkuu ametaja mapinduzi makubwa yaliyofanyika kwenye kila sekta nchini ikiwemo elimu; afya; nishati; mifugo; viwanda; barabara; viwanja vya ndege; uchukuzi wa anga; uchukuzi wa reli; uchukuzi wa majini; madini; sanaa za filamu na muziki; utalii na michezo mbalimbali. Amesema maafisa hao wanapaswa kuyatangaza mageuzi hayo.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMATATU, MACHI 18, 2019.
No comments:
Post a Comment