Waziri wa Habari, Utamaduni,
Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe, akisikiliza maelezo ya Meneja NMB Kanda ya Kusini, Janeth Shango, alipotembelea banda la benki hiyo
kabla ya ufunguzi wa Jukwaa la tisa la fursa za Biashara na Uwekezaji mkoani
Lindi.
Jukwaa hilo lililoandaliwa na
Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN) kwa kushirikiana na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
wa Lindi, liliwakutanisha washiriki takribani 350 wakiwemo wawekezaji,
wakulima, wajasiriamali, wafanyabiashara, taasisi mbalimbali na viongozi mbalimbali
wa serikali.
Benki hiyo imefanya vizuri katika
sekta ya kilimo na kwa kutoa mikopo kulingana na mnyororo mzima wa zao husika
kupitia matawi yake 7, pamoja na kutoa huduma zingine za kifedha kupitia
mawakala zaidi ya 105 na mashine za kutolea fedha za ATM mkoani humo.
Kwa upande wake, Meneja
Mwandamizi wa Biashara ya Kilimo wa benki hiyo Carol Nyangaro alisema katika
benki hiyo ambayo serikali ina hisa ya asilimia 30 kupitia bodi ya mikopo
iliidhinisha kiasi cha shilingi bilioni 500 kwa ajili ya mikopo ya wakulima na
tayari shilingi bilioni 450 zimetumika.
Meneja
Mwandamizi wa Kilimo Biashara wa Benki ya NMB, Carol Nyangaro akitoa mada
baada ya ufunguzi wa Jukwaa la tisa la fursa za Biashara na Uwekezaji mkoani
Lindi.
NMB ni benki inayotambua kuwa
kilimo ndio uti wa mgongo nchini kwani asilimia 75 ya watanzania
wanajishughulisha na kilimo na hivyo itaendelea kuwekeza zaidi katika kilimo.
No comments:
Post a Comment