HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

March 28, 2019

NI VITA YA AZAM, KAGERA SUGAR KESHO KAITABA

NA JOHN MARWA

MATAJIRI wa Jiji la Dar es Salaam, AZAM FC kesho watashuka katika Dimba la kaitaba kusaka nafasi ya kutinga nusu fainali kombe la Shirikisho dhidi ya Kagera Sugar.

Mratibu wa Azam FC, Philip Alando amesema wanatambua ushindani uliopo na namna ilivyo kazi kupata matokeo ila wana imani kubwa ya kusonga mbele kwenye miashindano hayo.

"Hatuna cha kuhofia, tuna wachezaji wazuri na wapambanaji kila idara na Imani kila mmoja atatatekeleza majukumu yake vilivyo, nia yetu ni kupata matoko chanya ili kusonga mbele kwenye hatua ya nusu fainali.


"Hii ni vita ya ushindi kwa kila mmoja, ni wazi atakaye poteza pambano hili atakuwa amejirupa nje ya mashindano jambo ambalo linaufanya mchezo kuwa fainali kwani hakuna anayetafuta sare.alisema Alando


Baada ya mtanange huo Azam watalazimika kusalia kanda ya ziwa kwa ajili ya mchezo wa ligi kuu Tanzania bara TPL.

No comments:

Post a Comment

Pages