Rais
mstaafu wa Awamu ya Nne, Jakaya Kikwete akizungumza na baba mzazi wa
Ephraim Kibonde, mzee Samson Kibonde, alipokwenda nyumbani kutoa pole
kwa familia.
Jeneza lililokuwa na mwili wa aliyekuwa mtangazaji wa Clouds
Media, Ephraim Kibonde, likiwa katika matayarisho ya kushushwa katika
nyumba yake ya milele. Kibonde alizikwa katika makaburi ya
Kinondoni jijini Dar es Salaam.
Mama mzazi wa Ephraim Kibonde akiwasili katika makaburi ya Kinondoni.
Watoto wa Ephraim Kibonde wakiweka shada la maua katika kaburi la baba yao.
Wabunge
wakiweka kwa pamoja shada la maua katika kaburi la Ephraim Kibonde .
Kutoka kushoto ni Mbunge wa Mtama, Nape Nnauye (CCM), Mbunge wa Kigoma
Mjini, Zitto Kabwe (ACT-Wazalendo) na Mbunge wa Mikumi (Chadema), Joseph
Haule ‘Prof J’ .
Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP, Dk. Reginald Mengi pamoja na mkewe wakiweka shada la maua katika kaburi la aliyekuwa mtangazaji wa Clouds Media, Ephraim Kibonde.
No comments:
Post a Comment