Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Mh. Said Mtanda (aliyeshika tofali) akitoa maelezo kwa Mkuu wa mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo wakati wa ziara fupi ya kuangalia maendeleo ya ujenzi wa hospitali ya Wilaya hiyo ulioanza mapema mwaka huu na kutakiwa kumalizika mwishoni mwa mwezi wa sita mwaka 2019.
Na Mwandishi Wetu
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa
Mh. Joachim Wangabo amewaagiza wakuu wa Wilaya za Mkoani Rukwa kuhakikisha
wanakuwa na utaratibu wa pamoja katika kutembeleana na kuelezana changamoto na
mafanikio katika maeneo ya mradi wa ujenzi wa hospitali za wilaya ili kujenga
hospitali hizo katika hadhi sawa na hatimae kupeana ujuzi wa utekelezaji wa
mradi huo.
Amepongeza ushirikiano
unaoonyeshwa na uongozi wa wilaya ya Nkasi unaoongozwa na Mkuu wa Wilaya hiyo
mh. Said Mtanda pamoja na wabunge, madiwani na mkurugenzi na kusifu mafunzo
waliyoyapata na kuyarekebisha wakati wa utekelezaji wa ujenzi wa vituo vitatu
vya afya katika wilaya hiyo na kuonyesha dalili za kutojirudia kwa makosa waliyoyafanya
wakati wakitekeleza ujenzi wa vituo hivyo.
“Wakuu wa Wilaya waweke
program ya kutembeleana kwa pamoja ili kujifunza, wanakuja kwa mfano (wilaya
ya) Nkasi, wanakwenda wilaya ya Sumbawanga, Wanakwenda wilaya ya Kalambo halafu
watakaa chini wafanye tafakari ili waone ni namna gani wanweza wakasimamia
vizuri hizo hospitali zetu za wilaya kwasababu tunapaswa tuwe na kitu bora,
hospitali zote tatu ziwe bora ndani ya mkoa wetu,” Alisisitiza.
Alisema kuwa halitakuwa
jambo jema kwa wilaya moja kuwa na ufanisi sana ilihali wilaya nyingine inakuwa
na changamoto na hivyo vyema wakaungana kama timu na kutembelea miradi hiyo ya
ujenzi wa hospitali za wilaya ili kila mmoja aweze kujifunza kutoka kwa
mwenzie.
Ameyasema hayo baada ya
ziara yake ya kutembelea ujenzi wa hospitali ya Wilaya ya Nkasi pamoja na
ujenzi wa hospitali ya Wilaya ya Sumbawanga ili kujionea changamoto mbalimbali
zinazoukabili mradi huo ambao unatakiwa kuisha mwishoni mwa mwezi wa sita mwaka
huu.
No comments:
Post a Comment