Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), Elia Madulesi, akizungumza wakati akimkaribisha Postamasta Mkuu wa Shirika hilo, Hassan Mwang'ombe (kulia), kuzungumza na waandishi wa habari kuelezea mkakati wa shirika katika kuimarisha maduka yake ya kubadilishia fedha za kigeni nchini. Katikati ni Meneja Mkuu Uendeshaji Biashara wa TPC, Mwanaisha Said.
Baadhi ya Maofisa wa Shirika la Posta wakiwa kwenye mkutano huo.
Baadhi ya Maofisa wa Shirika la Posta wakimsikiliza Postamasta Mkuu, Hassan Mwang'ombe, wakati akizungumza na waandishi leo jijini.
Postamasta Mkuu, Hassan Mwang'ombe, akizungumza kwenye mkutano huo. Kulia ni Meneja Rasilimali za Shirika, Macrice Mbodo na kushoto ni Meneja Mkuu Uendeshaji Biashara wa TPC, Mwanaisha Ali Said.
Postamasta Mkuu, Hassan Mwang'ombe (katikati), akuzungumza na waandishi wa habari kuelezea mkakati huo wa shirika.
Baadhi ya wateja wakipata huduma kwenye maduka ya kubadilishia fedha za kigeni ya Shirika la Posta leo, Ofisi ya Posta Kuu jijini Dar es Salaam.
Wateja wakiwa katika Kituo cha huduma mbalimbali za shirika wakisubiri kupatiwa huduma, Ofisi ya Posta Kuu jijini Dar es Salaam leo.
Moja ya maduka ya kubadilishia fedha za kigeni ya Shirika la Posta, jijini Dar es Salaam.
Tarehe 28 february 2019 Benki kuu ya Tanzania ilitangaza kwamba maduka ya kubadilishia fedha yatabaki kwenye mabenki, taasisi za kifedha pamoja na maduka ya fedha za kigeni za Shirika la Posta Tanzania tu.
Tunapenda kuutarifu umma wa watanzania kuwa Shirika la Posta limejizatiti katika kutoa huduma hiyo kwa umma wa watanzania na tunapenda kuwajulisha kuwa mpaka sasa tunavyo vituo kumi (10) vinavyotoa huduma ya kubadilisha fedha ambapo ni Kariakoo, Posta Mpya, Kijitonyama, Oysterbay, City drive (Sokoine ) , Libya Posta, Uwanja wa ndege, vituo hivi vyote vipo jijni Dar es Salaam na mpaka ifikapo tarehe 15 Marchi 2019 tutakuwa na vituo ishirini(20) vya kubadilishia fedha za kigeni.
Pia tuna mikoa miwili ambayo tayari huduma hii imeanza nayo ni ofisi kuu ya Posta Zanzibar na Arusha, Pia tunatarajia mwishoni mwa mwezi Marchi mikoa 17 yenye ofisi za posta zitaanza kutoa huduma hiyo. Tungependa kuutaarifu Umma ,watembelee katika vituo vyetu vya posta kupata huduma hii ya ubadilishaji fedha za kigeni.
Shirika la Posta Tanzania linapenda kuujulisha Umma kupokea taarifa hii muhimu kwao na kwa maendelea ya Taifa.
No comments:
Post a Comment