Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Tigo Tanzania Simon Karikari (wa pili kulia)
akikata utepe kuashiria kumkabidhi rasmi nyumba mzee Joram Mollel (93) ambaye
amekuwa akishiriki mbio za Tigo Kili Half Marathon kwa miaka minne mfululizo.
Kulia kwake ni mzee Mollell akifautiwa na mwanaye Elibarik Mollel pamoja na Afisa
Biashara Mkuu wa Tigo Tarik Boudiaf. Hafla hiyo ilifanyika mwishoni mwa wiki katika eneo
la Mushono jijini Arusha. Kulia ni kaimu Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Kaskazini,
Aidan Komba.
Babu Joram Molle (93) akitoa neno la
shukrani muda mfupi baada ya kukabidhiwa nyumba na Kampuni ya Tigo kutokana na
ushiriki wake wa mbio za Tigo Kili Half Marathon kwa miaka minne mfululizo.
Wanaomsikiliza kushoto ni Mkurugenzi
Mtendaji wa Tigo Simon Karikari akifuatiwa na Afisa Biashara Mkuu Tarik
Boudiaf, na kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Kaskazini Aidan
Komba. Hafla hiyo ilifanyika mwishoni mwa wiki katika eneo la Mushono
jijini Arusha.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Tigo
Tanzania Simon Karikari, akimkabidhi fungua za nyumba mzee Joram Mollel ikiwa
ni kama zawadi na kukubali mchango wake kwa mbio za Tigo Kili Half Marathon kwa
miaka minne mfululizo pamoja na umri mkubwa. Anayeshuhudia ni Kaimu Mkurugenzi
wa Tigo Kanda ya Kaskazini Aidan Komba. Hafla hiyo ilifanyika mwishoni mwa wiki
katika eneo la Mushono jijini Arusha.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Tigo Simon
Karikari akizungumza na wahabari hawapo pichani wakati wa hafla ya kumkabidhi
nyumba Mzee Joram Mollel (93), aliyekuwa akikimbia mbio za Tigo Kili Half
Marathoni kwa miaka minne mfululizo, kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya
Kaskazini Aidan Komba. Hafla hiyo ilifanyika mwishoni mwa wiki katika eneo
la Mushono jijini Arusha.
Baadhi ya wafanyakazi wa Kampuni ya Tigo
Tanzania wakiwa katika picha ya Pamoja muda mfupi baada ya Kampuni hiyo
kumzawadia nyumba mzee Joram Mollel mkazi wa Jijini Arusha ikiwa ni kutambua
mchango wake katika mbio za Tigo Kili Half Marathon ambazo mzuee huyo
ameshiriki kwa miaka minne mfululizo. Hafla hiyo ilifanyika mwishoni mwa wiki
katika eneo la Mushono jijini Arusha.
Na
Mwandishi Wetu, Arusha
KAMPUNI
ya Mawasiliano ya Tigo imemkabidhi nyumba ya vyumba 17 ikiwa na samani zote za
ndani Babu Joram Mollel (93), kutokana na ushiriki wake wenye mafanikio katika mbio
za Tigo Kili Half Marathon kwa miaka mine mfululizo.
Hafla
ya makabidhiano hayo ilifanyika eneo la Mushono nje kidogo ya Jiji la Arusha,
ikiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Tigo Simon Karikari pamona na Afisa
Biashara mkuu Tarik Boudiaf
Akizungumza
kwenye hafla hiyo Karikari alisema, nyumba hiyo ilinunuliwa na kukarabatiwa
kisha kumkabidhi Babu Mollel kama ishara ya shukrani kwa kujituma na umahiri
wake katika riadha.
'Babu
Mollel amekuwa akishiriki mashindano ya Tigo Kili Half Marathoni kwa miaka
mingi sasa. Tulipoona hali ya makazi yake si nzuri Tigo tuliona njia sahihi ni
kuwezesha apate nyumba yake mwenyewe,"alisema Karikari.
“Katika nyumba yake hii ya hapa Mushono, Babu
atakuwa anakaa katika nyumba ya kisasa, iliyo tayari na samani pamoja na vyombo
vyote muhimu vya ndani. Nyumba hii pia imeunganishwa na umeme na maji. Hati ya
nyumba pia ipo kwa jina lake, hivyo yeye ndiye mmiliki halali wa nyumba hii,”
aliongeza Karikari.
Aidan Komba, ambaye
ni Kaimu Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Kaskazini alisema kwamba nyumba
imegawanyika sehemu tatu na kuongeza kuwa Babu Mollel atakaa katika nyumba moja
na mbili zilizobaki ataweza kuzipangisha na kujipatia kipato cha kuendeshea
maisha yake ya kila siku.
“Napenda
kuwashukuru sana Tigo kwa zawadi hii ya kipekee. Maneno yangu hayawezi kuelezea
furaha niliyonayo. Ktendo hiki kina maana kubwa sana kwangu. Maana hivi sasa
ninaweza nikasema sasa nina mahali pakuita kwangu,” alisema Babu Mollel.
Ushiriki wa Babu
Mollel katika mashindano ya Kilimarathon ni wa zaidi ya miaka 15, ambapo
amekuwa akiwavutia watu wengi kumshangilia wakati akishiriki mbio za marathon,
pamoja na uzee wake. Katika miaka minne mfululizo iliyopita, Tigo imekuwa mlezi
na mdhamini mkuu wa mbio za kilometa 21 zinayojulikana kama ‘Tigo Kili Half-Marathon’,
ambayo ni nusu ya mbio kamili ya kilometa 42 za marathon ambayo hufanyika
katika vilima vya Mlima Kilimanjaro, mlima mrefu kuliko wote barani
Afrika.
“Babu Mollel ni taswira halisi ya uanamichezo,
ujasiri na jitihada. Yeye ni mfano aliye hai kwamba kama binadamu tunaweza tukafanikiwa
katika lolote lile ambacho tukiamua kukifanya kwa dhati, na kuondoa dhana nzima
kwamba umri au changamoto zingine zozote zinaweza zikawa sababu ya
kutokufanikiwa kwetu. Leo, tunamsheherekea yeye,” alieleza Karikari kuhusu mzee
huyo wa miaka 93.
Mwaka jana, Tigo
ilishirikiana na Babu Mollel katika kampeni maalum ya Tigo Kili Half-Marathon
iliyoitwa ‘Tisha kama Babu’. Kampeni hiyo ilikuwa na lengo kubwa la kuhamasisha
Watanzania kuweza kuishi maisha ya kujali afya zao. Wakati huo huo, Tigo pia
ilisitisha rasmi namba ya mbio aliyokuwa akiitumia Babu Mollel ‘1040’ na
alitambuliwa rasmi kama mwanamichezo wa heshima ‘Hall of Fame’.
No comments:
Post a Comment